Ushauri: Naomba kujuzwa namna ya kuongeza kimo/ urefu wa gari

kasulukasulu

New Member
Joined
Oct 5, 2013
Posts
3
Reaction score
3
Salam wakuu,

Nimekua mtumiaji wa magari yaliyo chini. Nilianza kutumia Toyota RunX na sasa natumia Subaru imprezza. Katika matumizi yake nimekua napata changamoto ya kimo chake ikiwemo kuharibu mabampa.

Zaidi ya mafundi wawili wamenishauri kupandisha/ kuongeza urefu wake. Naomba mawazo yenu kama kuna changamoto zozote za kufanya zoezi hili na mambo ya kuzingatia ili niongeze bila kuathiri vitu kama balance ya gari.
 
Kwanza unapoadjust driving height kuelekea juu maana yake unaongeza center of gravity na pia unaongeza lift force as more air will be flowing in underbody. Hii inaweza kuwa na athari kwenye moments mbalimbali zinazotokea wakati gari inatembea kama Yaw, rolling e.t.c. Usishangae siku unataka kudrift ukajikuta uko chini.

Pia inategemea na aina ya Aina ya gari, aina ya suspension na overall flexibility ambayo gari yako inaoffer.

Kuna heights ndogondogo unaweza kuadjust, mfano badala ya kutumia low profile tires unaweza kutumia high profile tires japo sometimes yanaweza kuwa yanakwangua hasa wakati wa kukata corner.

Sijajua subaru impreza kama inadrive nyuma au mbele. Ila kama inadrive mbele, ukiongeza urefu mbele lazima huo urefu utaathiri overall tyre life, grip pamoja branking.

Mwisho sishauri sana mtu kucheza na dynamics za driving height ya gari unless kama huyo mtu ni expert na anajua anachokifanya. na sio hawa mafundi nyundo.
 
Binafsi napinga sana mambo ya kuinua gari. Lakini kwa uhalisia wa maeneo tunayoishi na barabara za kuelekea huko, kuinua hizi gari zetu za chini hakuepukiki hata kama wewe ni dereva mzuri namna gani. Jitu katoa option nzuri ya kuinua.

Ila kama hutoona taabu kupanda bodaboda wakati una gari limepaki ndani, then usiinue.
 
Mazingira tunayoishi yanatulazimu kunyanyua magari lakini si jambo la busara hata kidogo, ile balance halisia ya gari inapungua, muonekano wa gari unapotea..
tena hiyo subaru impreza ikinyanyuluwa inakuwa mbaya sana...

Ni kagari kazuri ila walikatengeneza chini sana bora hata passo..
 
Mie nimekuwa mbishi mpaka leo. Iko vile vile. Ila ndio hivyo, bodaboda zinahusika saana 🙂 🙂.
 
Shukrani wadau, nimepata somo zuri kutoka kwenu. Mpaka sasa mzani umelalia kwenye kutolipandisha. Chakufanya muda wa kubadilisha matairi naweza kuchukua ya saizi kubwa kuliko yaliyopo, hii nitaifanya kwa ushirikiano na fundi ili kusiwe na changamoto kama za kugusa bodi muda wa kukata kona.
 
Salam wakuu,

Nimekua mtumiaji wa magari yaliyo chini. Nilianza kutumia Toyota RunX na sasa natumia Subaru imprezza. Katika matumizi yake nimekua napata changamoto ya kimo chake ikiwemo kuharibu mabampa.

Zaidi ya mafundi wawili wamenishauri kupandisha/ kuongeza urefu wake. Naomba mawazo yenu kama kuna changamoto zozote za kufanya zoezi hili na mambo ya kuzingatia ili niongeze bila kuathiri vitu kama balance ya gari.

Hii gari ni changamoto kwa kweli
 
Mimi natumia Toyota Allex niliinunua mwaka 2016 mwishoni, mwanzo nilipata nayo shida sana nilikuwa najisikia vibaya sana ilivyokuwa ikigonga kwenye matuta, but tangu nilipoamua kupandisha gari sijawahi kujuta, niliongeza zile rubber nusu inch na kupata matyre ya high profile basi tatizo likaisha na nilishasahau. Hakuna kitu kinakera kama unaendesha gari umempa mtu lift halafu gari inagonga kwenye matuta
 
Hakikisha unaliweka sehemu yenye mwanga wa kutosha,unaweka oil nzuri na mafuta masafi. Pia uwe una ipark sehemu yenye rutba.

Back
Top Bottom