wazo lako ni zuri sana,
naomba nichangie machache kwenye wazo lako na wengine watajazia. Kwanza tafuta eneo kubwa kama eka tatu mpaka nne hivi katika mkoa wa Pwani hasa wilaya ya Bagamoyo na Kisarawe, ukiweza along Morogoro Road. Hapo mahali weka mazingira ya kiasili kabisa, katika eneo hilo utaweka workshop ndogo ya mizinga, mizinga yenye nyuki wadogo ipate sehemu, nyuki wakubwa wapate sehemu kama maeneo ya kufundishia.
tenga jengo dogo la kuweka mashine za kufundisha namna bora ya kukamua asali kitalaamu na uwe na ukumbi wa kufundishia pia. Ukikamilisha hayo, tengeneza vipeperushi na ufungue duka lako kama utakavyo. Kama unaweza, kituo hicho kafungulie Dodoma, Singida, Iringa au Mby.