Ushauri: Nataka kumshitaki Ndugu yangu kwa makosa ya mtandaoni

Ushauri: Nataka kumshitaki Ndugu yangu kwa makosa ya mtandaoni

Shy land

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2013
Posts
6,208
Reaction score
2,767
Nimekasilishwa sana na ujumbe ambao anaendelea kuusambaza huyu ndugu yangu unaohusu masuala ya siasa.Binafsi sijapenda tabia anayoifanya. Ametumia sms ya kumkashifu Rais wetu ajae, eti anasema.

"Hakuna cha MAGUFULI wala MAKOMEO,
CCM ni walewale sema tu wamebadili chupa lakini pombe ni ilele.Kura zangu zote kuanzia udiwani, ubunge na urais ni UKAWAAAAAAA tu, hakuna la ziada, CCM mpaka hapo wametufikisha pabaya sana.
sasa tusemeee! yatoshaaaaa kwa sauti tukianzia na wewe.

Forwad sms hii kwa makamanda 90 ili tupate ushidi wa kishindoooo!"

Hapo ndio wisho wa sms inayosambaza chuki kubwa kwa wanainchi.

Watanzania naombeni ushauri, huyu ndugu yangu ninataka kumshitaki ili nchi yetu iendelee kuwa na amani.

Hatuwezi kukubali watu wajinga kama ndugu yangu waichome amani yetu.
 
Hiki kizazi cha Sasa kimechokuta mitandao ya Kijamii,wengi wao uwezo hata wa Kufikiria ni Mdogo na kuona woote humu JF ni watoto wa Nursery.

Hembu wapunguzieni Mod kazi za kufanya.Sio kila upuuzi kuuleta humu.

Nakumbuka kuna mzee aliwahi kuniambia Kizazi cha sasa wengi watakuwa na Uelewa mdogo sana na kupoteza kumbukumbu kutokana na kubeba ujinga mwingi kichwani kuliko kubeba mambo ya maana.

Mleta uzi tafuta watoto wenzio
 
Kweli nimeamini walivyosema...
Heri kufa macho kuliko kufa moyo
 
magufuli ashashnda tayari chadema wamempitisha fisadi mkuuu.mageuzi yamesalitiwa na kufika hapa tens ni fifty years to come
 
Utawezaje kuchota maji bombani ukamwage baharini mafuriko hayazuiliki mzeee
 
Hayo ni maneno ya kawaida saana kwenye kipindi kama hiki. Kama umeweza kustaajabu ujumbe huo, subiri kipindi cha kampeni kianze utaduwaa mwenyewe na utakayoyasikia kuhusu wagombea wote.
 
Back
Top Bottom