Ushauri: Nataka kununua gari hii

Mkuu, kwanza hiyo sio New Model. Hiyo ni 2nd Generation Vitz.

1st Generation ilikua 1999 hadi 2005.

2nd Generation ilikua 2005 hadi 2010...
Bado hadi hapo sinunui wakipanda watu wanene wanne haliwezi kupanda mlima duuuu nunua bajaji ufanyie biashara
 
Ina namba za ubalozi zile za bluu.

ooh kwa maana hiyo ni kwamba hiyo gari ilisajiliwa kwa msamaha wa kodi, kwa sababu huyo mmiliki ni afisa balozi wa ubalozi fulani. Kumbuka kwa mujibu wa sheria anayepata msamaha wa kodi ni mtu/milimiki sio gari.

Kwa hiyo mmiliki akibadilika(kwa mfano wewe unaponunua gari hili) inatakiwa ulipe kodi (kwa sababu wewe hukidhi vigezo vya msamaha wa kodi kama ilivyo kwa afisa ubalozi husika) kutokana na current value ya hilo gari kwa sasa(sio kwa value iliponunuliwa wakati inaingia nchini).

Afisa wa TRA ataweza kukokotoa kodi kulingana na thamani ya gari kwa sasa(depreciated value)

Nakushauri uwaone watu wa TRA kabla hujafanya maamuzi ya kununua gari.
 
Cc 1270 unauliza ulaji wa mafuta basi nunua t-better motorcycle itakufaa
Watu tuna Corolla ya 1995 ina 1498CC na haili mafuta tunapeta sasa hii akiuliza tena ya 2007 inabidi umshauri achukue zile za Zenji tukutuku...by the way anahitaji kujifunza maana ndo usafiri wake wa kwanza hivyo asijali sana kuhusu mafuta hiyo ipo poa maana gari la kwanza hutakiwi kununua gari complicated
 
Thanks mkuu, kwa maana nyengine hii kwa kujifunzia kumiliki gari inanifaa au sio?
 
Asante mkuu
 
Hiyo bei ya USD 2600 in sawa na Tz sh milioni 6 hivi,gari za ubalozi hazijalipiwa ushuru,ukiweka na ushuru na usajili aandae milioni 6 nyingine na hivyo kununua ako kagari kwa milioni 12 hivi,si bora aagize Raum au gari nyingine kubwa kwa hela hiyo?
 
Kaka. gari yenye 60000km ya mjapan na wa huku ni tofauti kabisa kama mpya. Kama umeridhika nayo ichukue.
 

Sounds like 'TANGAZO'.

-Kaveli-
 
achana nalo hilo labda kama wewe ni diplomat
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…