Ushauri: Nataka kupita Mikumi mbugani na BAJAJI

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
2,567
Reaction score
416
Wakuu,

Kesho jumatano natarajia kwenda Kyela, Mbeya lakini usafiri nitakaoutumia ni pikipiki ya tairi 3 yaani bajaji, na nitapita nayo pale mbugani Mikumi kwa kasi ya roketi, natumaini hakuna mnyama atakaenizingua mbugani.

Wakuu mna ushauri wowote hapa?
 
Huwezi kutoka Dar na Bajaji mpaka Mbeya.....hicho kibajaji kitalipuka moto.
 
kusafiri umbali mrefu siyo tatizo kuna mshkaji alitoka sumbawanga hadi dodoma na familia yake, na kurudi wiki iliyofuata, ila kwa suala la mikumi nadhan ukipita mchana hakuna noma. ubaponyeghe abha ngonde
 
Kasi ya rocketi sasa tukushauri nn tena na ushasema hakuna mnyama atakusogelea
 
Kuna kichaa alikuwa anakatiza kwa miguu mbugani na hakuliwa! All the best, safe journey
 
Wasiwasi wako tu simba wa mikumi hawana tabu kabisa tena nakushauri ukifika hapo mbugani ikokote tu hiyo bajaj yako watakuangalia tu hawatakufanya chochote

mkuu asante kwa ushauri
 
kusafiri umbali mrefu siyo tatizo kuna mshkaji alitoka sumbawanga hadi dodoma na familia yake, na kurudi wiki iliyofuata, ila kwa suala la mikumi nadhan ukipita mchana hakuna noma. ubaponyeghe abha ngonde

sasa kama yeye kaweza mi nitashindwaje bana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…