Ushauri: Nataka kutoka nje ya Tanzania kutafuta maisha

Ushauri: Nataka kutoka nje ya Tanzania kutafuta maisha

Mangole Valles Michael

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2021
Posts
338
Reaction score
683
Wakuu habarini za leo?

Nikiwa kama muumini ninae amini maisha ni popote, Leo nimeleta Uzi huu nikiwa na lengo la kupata mwongozo kwa walio nitangulia kutoka nje ya Tanzania au walio na uzoefu wa nchi zingine barani Africa au nje ya Africa.

Kwanza kutoka nje ya Tanzania kwenda ku-make life abroad ni ndoto yangu tangu nikiwa mtoto na kwasasa naona umri wa kuiishi ndoto yangu ni Sasa.

Hivyo basi naombeni mwongozo ni nchi gani ambayo unaweza nishauri kwenda kwa ajili ya utafutaji wa maisha kulingana na fursa za nchi husika? Pamoja na mwongozo wa kufika huko.

Mimi kama Mimi nchi ambazo nimekua nikiwaza kwenda nchi ambazo ni visiwa kama sheli sheli (Seychelles) Mauritius n.k
-kwa south Africa sipapi kilaumbele Sana may be Botswana na kwingine.

Kwa wale mtakao shauri kua Tanzania kuna fursa nyingi kuliko nje sikatai ni kweli zipo ila kama una mchongo nipatie nipige, kama na wewe una fursa za mdomoni bas naomba utulie.
 
Hakikisha una vitu vifuatavyo:

1. All legal documents, such as VISA, Passport, etc

2. Relatively enough money (kwa wengine kiasi hiki ni sawa na kile ambacho kingemtosheleza kama mtaji wa kuanzisha business yake hapahapa)

3. Consider suala la language unakoenda. Kwa mfano, ukitaka kwenda Ufaransa, walau ujue masuala ya Bonjour

4. Ukiwa na elimu/taaluma fulani ni added advantage. Vinginevyo jiandae kuwa mtumwa wa hiari kwa muda

5. Usisahau kuwauliza hao jamaa madini yenu mrabaha mbona wamesitisha kulipa tena!??? Karibu tena home, sawa!??? Usiwe kama Wanaijeria 🙂
 
Back
Top Bottom