Ushauri: Nataka kuweka curl kwenye nywele zangu

Ushauri: Nataka kuweka curl kwenye nywele zangu

Gods very own

Senior Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
124
Reaction score
66
Sweeties, nataka kuweka curl kwenye nywele zangu nina nywele ndefu zenye dawa ila mbele na nyuma zimekatika sana na sasa hivi zimeotea balaa, so nina mpango wa kuzipunguza ziwe saizi ya kitana alafu niweke curl;
Je itafaa?
Au nisubiri hadi nywele za dawa ziishe?
Je curl inaweza wekwa kwenye nywele fupi zenye dawa?
Na hua ina last mda gani?
Na je curl ina mafuta yake special au ukishatengeneza unaweza paka mafuta yoyote.
Na je curly hair zinatunzwaje?
 
Haya madawa ya nywele sio mazuri, yatakuja kukuathiri hapo baadae..ni bora unyoe tu nywele zako zibaki simple....Unamaliza gharama zako bure tu
 
mi navyojua siku hizi curl imeadvance sio kama zamani ukiweka ilikuwa na harufu sana. nyoa nywele za dawa then tafuta saloon nzuri mtu anayeweza kuweka curl akuweke. maana curl ina wataalamu haiwekwi kama dawa nyingine saloon. kuhusu mafuta nafikiri unapaka mafuta hata wanayopaka walioweka wave. unatafuta gel nzuri tu basi.
 
Ukitaka kuweka cark hakikisha nywele yenye dawa yoote imeisha imebaki natural vinginevyo utalia na moyo
 
Curl usiweke,,,niliwahi uliza saloon moja kusema curl shngap?? Nikaambiwa ni elfu 40 nikashangaaa kwann mana tushazoea dawa ilizidi sana 13,, akasema kwasababi curl ni mbaya sana na hata saloon wanazoweka curl ni chache(fuatilia)

Km unataka nywele ya dawa weka weave then nunua mafuta ya weave utapendeza sana tu,,curl sikushauri
 
Mi nijuavyo nowadays you can rock curls with your natutal hair,
Kuna set za mafuta unanunua na unafany mwenyewe hata nyumbani
 
Back
Top Bottom