Ushauri: Nataka niache kuajiriwa nijiajiri

WENYELE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,433
Reaction score
1,442
Wakuu
Nimekua mwajiriwa wa kampuni flani binafsi kwa muda wa miaka miwili sasa,nimepata uzoefu mzuri tu wa kuweza kuendesha firm yangu pia.

Nimefanya kazi na mwajiri wangu vizuri tu ila kwa siku kadhaa imetokea kama msuguano hivi basi nami mood ya kufanya kazi ikaisha,niko kwenye position ya technical (yaani jikoni),products zote tunazouza nimezibuni mimi (yaani methods of manufacturing na designing yote ni mimi).Sasa nataka nifungue biashara inayofanana na boss wangu ila ninataka ni base kwenye product ambazo hatengenezi yeye,bidhaa zenyewe ni natural fragrances and food flavours km vile Vanilla,strawbery,cloves,mint,ginger,cinnamon flavours.

Nataka niwe natengeneza mwenyewe afu soko langu nilikua na-target kwa
1.Watengeneza marashi na sabuni (cosmetic and perfume sector)
2.Bakery industries
3.Dairy industries
4.Hospitality sectors na
5.Domestic users.

Nina elimu ya chuo kikuu na hii ndio professional yangu lakini sijawahi kufanya biashara ya aina yoyote pia sina mtaji wa kugharamikia initial cost kwa sababu hii biashara inahitaji initial investment kubwa.

Sasa wakuu nakuja kwenu kuomba ushauri,nifanyeje ili niweze kufanikisha lengo langu? Nategemea nikipata pesa ya kuconstruct equipment kwa kuanzia,nitaajiri watu wa masoko na kuweza kuitangaza na kubrand product zangu.Technical na manufactural engineering nitasimamia mwenyewe,nahitaji nisajiri kwanza mawazo yangu km kampuni ili nianze utekelezaji

Vifaa ninavyohitaji ni vifuatavyo.
1.Essential oil extractor (steam distiller)
2.Spice grinder milling machine.
5.Flavour extractor equipment etc.
Raw materials nina-focus kufanya contract farming na wakulima wa viungo na vionjo wa vyakula.

Mfano,wakulima wa ginger (Tangawizi),mdalasini,strawbery,karafuu nk.
Kuhusu Soko naamini itakua ngumu mwanzoni ila nitatoboa badae maana kwa Tanzania hamna kiwanda kinacho-produce organic natural food flavours na viwanda vya maziwa vingi wanatumia sana artificial food flavours.

Naomba ushauri wenu na Mungu awabariki.
NB:Nahitaji ushauri kijasiriamali,huenda nikapoteza ajira yangu soon,sasa nimeamua kuchukulia positively hii changamoto
 
Nahitaji 4M tu mkuu ili nianze kuimpliment wazo langu
 
Ni kwel, mtaji unahitaji sh ngapi
Nimetafuta mashine online nimepata mashine ya kutengeneza essential oil za lemon grass,levender,ginger,cinnamon nk.
Tatizo sasa sina hela ya kununulia,nimeambiwa 2.5M kutoka china.
Nimewaza vitu vifuatavyo
1.Nitembeze bakuli kwa marafiki na washakaji zangu niwakope kuanzia 20K-30K kila mmoja,yaani nipitishe km mchango wa harusi ila sitawaambia km nachangisha sababu ya hii,nitawaambia nitairudisha ila hata nikishindwa project yangu iki-fail nadhani sitagombana nao maana ni hela kidogo.
2.Niende kwa mbunge wangu anikopeshe hela nitamrudishia.
3.Malipo yangu ya NSSF ila haya siyatarajii maana figisu figisu ni nyingi sana mwishowe nitakata tamaa na mradi wangu.
Naomba:Maoni yenu wadau
 
Hongera kwa Wazo zuri lazima uwe creativity mafanikio yanaanzia hapo. Usichoke kutafuta mtaji
 
Hongera kwa Wazo zuri lazima uwe creativity mafanikio yanaanzia hapo. Usichoke kutafuta mtaji
Asante mkuu,naomba mtu mwenye ujuzi wa kuandika proposal anisaidie,nataka nianze kwenda door to door kwa watu mashuri hasa wanasiasa
 
Changia kidogo niandae business proposal ya hiyo initiative!
 
Wazo lako ni zuri sana,ushahuri wangu sio kuzunguka na mawazo yako kwa watu wenyepesa ,mlango kwa mlango au kwa wanasiasa kama unavyodhani bali anza kidogo kidogo kwa kukusanya ,mfano mashine kisha,tafuta eneo n.k,vinginevyo kama unaanua kwenda kwa watu wenye pesa kuwa makini sana,maana kuna watu wana pesa hawana mawazo,mwishowe watakuomba andiko kisha walifanyie kazi wao.yameisha nikuta hayo mara 2.
 
Mkuu tuonane tuweze kujadiliana kuhusu kushare mtaji nipo tayari uaminifu hapa unatakiwa
 
Ilikuaje mkuu mpaka yakakukuta hayo
 
Wazo zuri Sana, utafanikiwa Sana, MI nafanya bakery, most ingredients nyingi zinatoka nje hapa bongo hakuna wazalishaji. Kama ukitengeneza products nzuri after few years utawakama wote. Cha msingi anzia popote ulipo kwa mtaji mdogo unagrow na unaweza Anza hata na products moja moja unapanda. Mitaji sometimes challenge. Anza hata nyumbani kufanyia shughuli utumie tools simple..
 
Mawazo yako hayo tayari we Tajiri nakushauri nenda taasisi za kukopesha na idea hiyo watakusaidia
 
Daah mpk uje upate mtaji tayari utakuta watu washa lifanyia kazi wazo lako.....japo haiwezi kua kikwazo....
 
umenikumbusha lile shindano la mengi kule Twitter
 
Unataka kutoka kwa tajiri lakini hauna mtaji?
Jipange sana wazo lako sio baya ila tafakari....
La msingi una ndoto nzuri inatakiwa isife big up wengi wamepitia njia hizo
 
Wazo zuri lkn hili la kuchangisha mmmh, nashauri utengeneze kampuni na utafute share holders
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…