lewis acid
Member
- Mar 21, 2017
- 57
- 120
Wakuu habari za majukumu.
Natambua JamiiForums ni kijiwe cha wasomi na mchanganyiko wa watu wenye busara zao.
Najitokeza mbele yenu mnipe ushauri kidogo, kwa ufupi mimi ni muajiriwa katika serikali yetu hapa Tanzania, kutokana na changamoto za kazi na hali halisi ya maisha nina plan kukopa fedha kiasi cha 10m kisha nianzishe miradi yangu binafsi ili nijiajiri niachane na kuajiriwa maana naona napelekeshwa ilihali maslahi ni duni sana.
Kazi ni nyingi mno na maslahi ni kiduchu sana, nilitamani kuanzisha miradi nikiwa katika ajira lakini muda ninaoingia na kutoka kazini ni wastani wa masaa 11 mpaka 12 kwa siku, hali hii inanichosha sana kiasi kwamba hata nikifika home akili inakua imechoka sana naishia kulala tu.
Kwa mantiki hiyo naona umaskini wangu unaweza kua wa kudumu maana hata nikiwatazama walionitangulia naona hawana kitu kikubwa sana walichofanya maishani.
Nina dreams nyingi na kubwa, napenda kua mtu huru na mwenye mafanikio makubwa kupitia biashara na kilimo, naiona ajira kama kifungo cha kunifanya niwe maskini. Sasa kwakua nimekaa kwenye system kwa takribani miaka mitatu naona ni vema nijilipue nikafanye yangu.
Naomba ushauri na mapendekezo yenu, watu hatulingani akili endapo unaona niko wrong basi naomba unishauri namna ya kuboresha hili wazo.
Kejeli na matusi sio mahala pake hapa, mimi ni kijana kama ulivyo kijana pengine nikawa sawa na mwanao ni vema unishauri kwa kujua unamshauri ndugu yako na mwana JF mwenzako.
Natanguliza shukrani.