Ushauri: Nataka nikope 10millions niache kazi serikalini, ili nijiajiri

lewis acid

Member
Joined
Mar 21, 2017
Posts
57
Reaction score
120
Wakuu habari za majukumu.

Natambua JamiiForums ni kijiwe cha wasomi na mchanganyiko wa watu wenye busara zao.

Najitokeza mbele yenu mnipe ushauri kidogo, kwa ufupi mimi ni muajiriwa katika serikali yetu hapa Tanzania, kutokana na changamoto za kazi na hali halisi ya maisha nina plan kukopa fedha kiasi cha 10m kisha nianzishe miradi yangu binafsi ili nijiajiri niachane na kuajiriwa maana naona napelekeshwa ilihali maslahi ni duni sana.

Kazi ni nyingi mno na maslahi ni kiduchu sana, nilitamani kuanzisha miradi nikiwa katika ajira lakini muda ninaoingia na kutoka kazini ni wastani wa masaa 11 mpaka 12 kwa siku, hali hii inanichosha sana kiasi kwamba hata nikifika home akili inakua imechoka sana naishia kulala tu.

Kwa mantiki hiyo naona umaskini wangu unaweza kua wa kudumu maana hata nikiwatazama walionitangulia naona hawana kitu kikubwa sana walichofanya maishani.

Nina dreams nyingi na kubwa, napenda kua mtu huru na mwenye mafanikio makubwa kupitia biashara na kilimo, naiona ajira kama kifungo cha kunifanya niwe maskini. Sasa kwakua nimekaa kwenye system kwa takribani miaka mitatu naona ni vema nijilipue nikafanye yangu.

Naomba ushauri na mapendekezo yenu, watu hatulingani akili endapo unaona niko wrong basi naomba unishauri namna ya kuboresha hili wazo.

Kejeli na matusi sio mahala pake hapa, mimi ni kijana kama ulivyo kijana pengine nikawa sawa na mwanao ni vema unishauri kwa kujua unamshauri ndugu yako na mwana JF mwenzako.

Natanguliza shukrani.
 
Biashara siyo lazima ufanye mwenyewe., while Ukiwa kwenye ajira anzisha biashara muajiri mtu wa kusimamia. Milioni kumi ni hela ndogo sana ambayo inaweza kuanzishia biashara usiyoijua from zero. Ila ungekuwa na experience na biashara yeyote ningekuwa wa kwanza kukushauri uache kazi, this is from real experience I have.
Endelea na kazi mkuu at the same time anzisha biashara after atleast two years baada ya kupita misimu mbali mbali ya biashara yako acha kazi.
Ni ushauri tuu
 
Ni jambo jema Sana kujiajiri ila nakushauri uanze hiyo biashara uliyopanga hata Kwa mtaji kidogo ili ukiona biashara yako imesimama ndio ukope kuongezea mtaji na ndio taratibu nyingine za kuacha kazi uzifanye Kwa sababu ukisema ukope hiyo pesa huku umeacha kazi alafu na biashara ikute ndo Mara yako ya kwanza kufanya, mkuu utayamani kukimbia nchi maana Kwa hali iliyopo inahitaji uweze kusoma soko kwanza kabla ya kujilipua kuweka pesa yote huko.

Yangu ni hayo tu
 
Hiyo hela inaweza ikawa ni nyingi sana kuanzia au kidogo sana inategemea na maisha unyoishi.
 
NAONA UNATAKA KUISOMA NAMBA KWA KUJITAKIA.KILA LA HERI MKUU
Acha kumkatisha tamaa

kizazi cha sasa sio kama cha zamani

wazee wetu ajira ndio zilikuwa maisha yao

siku hizi fursa ni nyingi sana ....acha fikra za

kitumwa ww.....dizain ww utakuwa karani

hiyo kada ni ngumu kujiongeza

(only fools do not change their mind)
 
mimi ningekushauri uache kazi kama hela ingekuwa ya kwako ume save.. na biashara unayoenda kufanya unaijua kwa experience sio za kuhadithiwa na watu....

kukimbia deni sio njia sahihi siku hizi kuna credit reference utakuwa kwenye backlist na itakuharibia sana kukopa mbeleni maana hata biashara isimame kama mengi kukopa hakuishagiiii...

njia sahihi ni fanya ufanyavyo upate experiwnce ya biashara wakati upo kazini tayariiiiiii...
 
Pole sana kwa huko ulipo,kwan unataka kuingiza sh ngp kwa siku ili uone maish afadhal kdg?umeshajipang kukabiliana na ushindnai huku nje?kabla ya kuanza biashara heb acha kaz kwanza ukae home miez mitatu halaf akili ikukae sawa then ndo uingie kwenye business.

Kuna mawili unaweza fanikiwa na ukayafurahia maisha pia unaweza kukwama na ukajuta.

Hua wafanyabiashara wadogo naokutan nao hua siwaambii wakakope ndio waanze biashara mara nying utakua na stress sana ila anza n aulichonacho baadae ukishaizoea buznes inakua rahis kukop na kuendeleza biashara. Inawezekana ukafanikiwa sana maanaa mtaj wa 10m ni mkubwa kw maneno lakin kuna sehem hta hela y frem kwa mwaka haitosh.

So cha kufanya anza na ulichonacho na ukitafutie uzoefu then ukikaa swa kopa.

Karib kwa ushuri zaid wa kibiashara hasa phone acessories hapa ndo mahala pake,
 
Una uhakika utaupata huo mkopo

What goes around always comes around
 
UKIKOPA na KUACHA KAZI huo mkopo utaulipaje? Si unatafuta kuolewa wewe?
Fanya hivi kama unakopa kwa kutumia mshahara hilo ni ruksa. Hiyo pesa iwekeze kwenye biashara. Ukifanikiwa kuendesha hiyo biashara baada ya mwaka mmoja bila kuyumba yumba ndipo ufikirie kuacha kazi. Kujiajiri sio rahisi kama watu wanavyosema...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…