Ushauri: Ni bora uendelee kupanga kuliko kununua kiwanja mabondeni

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
1,047
Reaction score
1,832
Huu ni ukweli mchungu,kama bado hujajichanga na kuweza kununua kiwanja kilicho sehemu salama ni bora uendelee kutafuta hela ya kuongezea ili kupata kiwanja eneo salama,watu wengi wameingia hasara kubwa Kwa kupenda urahisi.

Unakuta mtu anatangaza kiwanja TSH 500000 tena mjini na sisi kwa kupenda mteremko unakimbilia bila kuuliza historia ya eneo husika.

Mimi kama shuhuda wa hili miaka mitano nyuma kuna eneo nilifuatwa linauzwa tena kwa bei rahisi sana na hela nilikua nayo na nilikua na shida ya kiwanja, ila nilivyoenda kulikagua eneo nafsi yangu haikuridhika na nikasitisha kununua lile eneo.

Hivi ninavyozungumza jana usiku tulikua tunamsaidia jamaa kutoa vyombo nje na mpaka muda huu nyumba imeshaanguka yote

Wahenga walisema Rahisi huzaa ghali
 
Hakika, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Kwa hapa town ukitaka kulijua eneo fika kwenye kiwanja husika alafu ingia google map weka satellite mode alaf ujiangalie ulipo ukiwa bondeni utajijua tu na utaona jinsi mambo yalivyo
 
Back
Top Bottom