w0rM
Member
- May 3, 2011
- 81
- 192
Wakati Tanzania ikiendelea kujipambanua kuwa Nchi yenye maendeleo na mazingira mazuri ya kuishi, na Jiji lake la Dar es Salaam likijiandaa kuwa Jiji kubwa zaidi (lenye zaidi ya Wakaazi Milioni 10) ifikapo mwaka 2030, nadhani kuna mambo kadhaa muhimu ya kuzingatia kwa ajili ya maendeleo ya Dar es Salaam na Miji mingine.
Hebu fikiria baadhi ya maeneo maarufu zaidi duniani: Mitaa ya kihistoria ya Paris. Favela zenye rangi nyingi za Rio. Madaraja ya watembea kwa miguu yenye miundo ya kipekee ya Venice. Maeneo haya yanajulikana si kwa uzuri wake tu bali pia kwa upekee wake.
Tunapaswa kufanya nini? Kuna mengi, lakini mojawapo ninalodhani linafaa sana
Kuandaa mpango mkakati wa ujenzi kwenye miji inayoanza na kufananisha majengo kwenye miji ya zamani
Mambo ya urembo wa Makazi ni muhimu katika maisha ya kila siku ya Wakazi, yakichochea jinsi watu wanavyojisikia na mwingiliano wa maeneo yao. Ikiwa Miji inataka kuwavutia watu, lazima iwe mizuri.
Mapendekezo yangu ni kuwa Serikali kwa kupitia Wizara ya Ujenzi ianzishe Mpango Mkakati wa kuhakikisha Miji inayoanza kujengwa sasa kuna Miongozo ya ujenzi. Miongozo hii sio lazima kusema muundo wa nyumba itakavyokuwa ila ni vema kusema rangi ya nyumba inayotakiwa, rangi ya paa inayotakiwa, lakini pia nyumba ijumuishe nini katika mazingira yake ili kuweka muonekano wa mfanano katika eneo husika. Vya kujumisha inaweza kuwa mwonekano unaofanana wa sehemu ya Watembea kwa Miguu na Walemavu na vingine vingi.
Lakini pia, ni vema kuwa na miongozo katika miji hii kwa Mamlaka zinazohusika na huduma za Kijamii kama Umeme na maji ili kuweka miundombinu rafiki, hususan Mamlaka za maji kuweka miundombinu ya kupata maji (hydrants) kwa ajili ya kuzima moto. Itaokoa sana suala la kusema Zimamoto hawajaja na maji. Lakini lazima tukubali kwamba Miongozo hizi yote ina nia njema japo inabadilisha njia ambazo tulizoe kujenga nyumba zetu.
Tunapaswa kuweka mipango ya Miji inayojumuisha ushirikiano mzuri kati ya mamlaka za mipango, watoa huduma za umma, na wadau wengine kama vile wabunifu na wawekezaji. Hii itahakikisha kuwa maendeleo ya miundombinu yanalingana na mwelekeo wa ukuaji wa miji ambao tunatarajia.
Lakini pia Miongozo hii itoe Maelekezo kwa Miji iliyopo kubadili na kurekebisha majengo yake. Fikiria leo kwa Dar es Salaam tunasema nyumba za Wilaya kadhaa ziwe na majengo yenye rangi ya aina moja, uzuri wake utakuwaje?
Baadhi ya Miji yenye mpangilio wa rangi katika Majengo yake inayoonekana kwa kupendeza