Ushauri: Nifanyaje ili homemade pellets kwa ajili samaki ziweze kuelea

Tyrone Kaijage

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
1,617
Reaction score
3,405
Habarini wadau,

Katika kujifunza kwa ukaribu,ufatiliaji wa kukuza na kuwalea samaki aina ya Sato ambao nimechimba kijibwawa ka 40 sqm kwenye mazingira ya nyumbani kwangu kama darasa ili huko mbeleni niongeze mengine mpaka 6, kwa ulishaji nimekua natumia zile industrial floating pellets pekee.

Kuna mfugaji akanishauri pia kutumia uduvi alinambia kuwa samaki kuwalisha hii industrial food pekee watakua haraka ila hawawi watamu.

Katika kupekua pekua zaidi kwa mtandao nikakutana na maelekezo ya nutrients na aina ya ingredients ratio za aina za vyakula ambavyo vinaweza kukupa food formula mbalimbali za ulishaji samaki, mbali zaidi kuna taasisi zinaonesha pia unaweza ukatengeneza locally hizo floating pellets ila katika masomo yao naona wanaonesha mwanzoni ila results ya lengo la final product ( kuelea) hawaoneshi.

Nimejaribu mara kadhaa ila naona nafeli, natoa chakula ila mwisho wa siku kinakua denser than water hivyo kinazama.Niliweka vifaranga 300 wanaelekea mwezi 4 tangu October 10.

Je ni wapi naweza kuwa nakosea.

Ingredients? Ukaushaji? Au nini cha ziada kufanya chakula kiweze kuelea.

Ratio yenye nimetumia
Unga wa dagaa 25%
Unga wa pumba za mahindi 25%
Unga wa Soya 20%
Mashudu ya alizeti 15%
Vitamin ( Pig Mix) 10%
Unga wa muhogo/ Ngano 5%

Nilichanganyia cooking oil na maji kiasi kama nakanda ngano ya chapati

Kifaa nilitumia kile cha kusagia nyama cha mkono.

Nilikikausha siku 1-2 kwa jua la Dar.
 
Kuelea nazani kuna process inafanyika wakati wana zi heat na inatengeneza kama nafasi ndani, au chakula kina kuwa kama kina hewa kwa ndani,
 
Average density inatakiwa iwe ndogo kuliko density ya maji ndiyo vitaelea
 
Hata mimi niliwahi kupambana sana kupata jibu la hii suala, kuna aliyeshauri changanya mchanganyiko wako na unga wa wa ngano na uweke amira ili uumuke km process za kutengeneza maandazi (amira siyo nzuri kwa afya ya samaki)

Jibu sahihi ni hili haoa chini.......
Floating fish feed generally needs to be extruded, so that there is a gap inside the feed, and there is air in it to float, which is difficult for home handmade, it needs floating fish feed extruder machine.
Some people add baking powder to the grain material, I'm not sure if this kind of fish feed pellets is good for the growth of the fish, you can try if you have interests
 
Niliona haya maelezo katika mtandao wa Quora ila ni kama vile muwasilishaji hakuweka wazi juu ya hili gap la air na pia hii ya Amira kuna aleyesema 10% of the mixture inaweza kusaidia kuelea kwa 70% ila hakueleza madhara ya amira kwa afya ya samaki.
 
Kuelea nazani kuna process inafanyika wakati wana zi heat na inatengeneza kama nafasi ndani, au chakula kina kuwa kama kina hewa kwa ndani,

Inawezekana ni kama vinapulizwa or something like that, cause nimejaribu kufikiria pia kufanya reverse process ya industrial pellets from grains to powder then from powder to grains ili nione issue ni ingredients au processing.
 
Tafuta tu mashine Kwa ajili ya kaxi hiyo. Vipi samaki wako wamefikisha gram ngapi mpaka sasa?
 
Nimekuwa interested na hii mada nikaangalia Alibaba
Nimeziona machine nyingi za kutengeneza pellets na kuelea na bei zake sio mbaya inayegemea na ukubwa wa uzalishaji unaotaka

Kwa 350kg unapata kwa $2400 na zipo ndogo pia

Ila ni mradi mzuri kama unanunua hiyo machine na unazalisha na kuuza chakula cha samaki kwenye maduka

Acha nisubiri comments labda ntapata mawili matatu tena
 
Uli search kwa jina gani mkuu naomba details ili niende ku search na kusoma functioning yake
 
Niliangalia Alibaba kwanza, halafu nikaangalia YouTube pia
Screenshot_20230213_084348_Google.jpg
Screenshot_20230212_091133_Google.jpg
 
Back
Top Bottom