Ushauri: Niko kwenye transition period

Bill of Quantity

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
1,233
Reaction score
406
Habari zenu wadau wenzangu wa biashara na uchumi,

Ni kweli niko kwenye transition period, kutoka level moja ya kiuchumi, nahitaji kufika hatua nyingine!Mpango wangu uko hivi wadau, nimejiandaa na Tshs laki 4 net.

Nahitaji mawazo yenu bora ya biashara ili nichanganye na akili zangu hapa nilipo! Natafuta biashara ambayo naweza kuifanya, kama sole entrepreneur, biashara hiyo iwe na uwezo wa kuingiza si chini ya net profit Tshs elfu 40 kwa siku.

Lengo langu ni kwamba, baada ya miezi mitano niwe angalau na mtaji wa Tshs milioni 4+ nihamie hatua nyingine!
Kwa sasa niko Dar es salaam.
....................................
....................................
Mawazo yenu ni muhimu sana wadau, nahitaji michanganuo ambayo itatusaidia sote, si mimi tu.

Karibuni
 
Ngoja waje wataalam watoe idea zao.. Ila kwa haraka haraka laki 4 izalishe profit elfu 40 kwa siku, yan ndan ya cku kumi lak 4 imerud... Aisee naisubir kwa hamu hiyo idea kama ipo, wanasemaga kila kitu kinawezekana
 
Mkuu hyo net profit ya 40K kwa siku ni kubwa sana ukilinganisha na mtaji wa 400K. Hebu search humu jukwaani kuna thread nyingi sana zinazohusiana na kuanzisha biashara kwa wenye mitaji midogo kama wako. By the way HONGERA kwa kuamua kuwa mjasiriamali.
 
RadioActive

Kama DSM
Njia rahis fanya hivi, nenda mkoani tafuta vijana ambao hawana shughuli maalum 15 watafutie vyumba maeneo ambayo vyumba ni bei rahisi....nenda kariakoo...tafuta zile birika zinazotumika kuchemsha na kuzungusha kahawa mtaani.

.wape vijana ukikomaa saana wakupe 10,000/kwa siku,ukiwanea huruma saana 5,000...baaada ya miezi 05 waachie hiyo biashara wewe utakuwa ushagraduate kufanya biashranyingine, all the best
 
Last edited by a moderator:
Fanya black market kwny boarders za Tanzania kwa mfano. KASUMULU-songwe malawi.
Unanunua kwacha sehemu ambayo iko chini zaidi kwa pesa yako mfano. 400,000 Unanunua kwacha kwa mchanganuo ufuatao.
1MWK(Malawi kwacha) = 4.2 Tshs hapo umenunua kwny byuro ambayo ina viwango vya chini ambayo utaitafuta au hata kwa wanaoingia toka malawi lbda kwa haraka haraka atakuuzia kwa 4.1.
Then naww utakuja kuuza kwa wanaoenda malawi kwa 4.3 MPAKA 4.4.

1mkw=4.2Tshs
xmkw=400,000Tshs

(400,000 * 1)/4.2=x

x= 92,238.0952MKW
Utakua na mtaji mdogo wa KWACHA 92,238.0952 ambapo ukifanikiwa kuziuza zote kwa mteja mmoja kwa rate ya 4.349inamaana utapata
92,238.0952* 4.349 = 414,190.476 Inamaana umepata faida elfu 14 then unannua fasta.
kwa muda wa siku ukihudumia wateja 5 kwa rate iyo maanake 14000*5=70,000 Tshs per day.

kwa mwezi ni 70,000 * 26=1,820,000 Tshs
nadhani hapo utahama toka stage moja kwenda nyingine.

ANGALIZO;
Kuuza pesa ya kigeni kwa wateja itategemea ujanja wako kwa wateja kwani mipakani watu wengi huogopa kutapeliwa, ivyo basi weka mazingira marafiki kwa mteja ili akujengee uaminifu na aweze kuikubali business yako.
Kununua /kuuza pesa ya kigeni muda ambao boda zinafungwa au kufunguliwando muda mzuri kwani wateja wengi wanakua kwny haraka ya kuwahi kuvuka ivo basi utaweza kufanya biashara yako kwa viwango vyenye faida

ONYO:
SI VIZURI KUTOKUWA MUAMINIFU KATIKA BIASHARA HII KWANI UNAPOMUUZIA MTU FAKE NADHANI HATA MUNGU HAPENDI HIVYO BASI SWALA LA KUENDELEA KWAKO LITAKUA NI GUMU SANA

NI USHAURI TU
ASANTE
 

Kaka nashukuru kwa ushauri mzuri.
Nazidi kukusanya mawazo mkuu.
 
ajam ally, shukrani sana kwa ushauri mzuri.
Nazidi kuangaza mawazo mkuu, kama una idea nyingine unaweza nitumia vile vile..
 
Last edited by a moderator:

Hii biashara inalipa sana ,kuna dogo muuza kahawa tuliwahi kumuuliza akatuambia kwa siku huwa anaingiza 16,000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…