Wadau habari!nimekuja kwenu kuomba ushauri,baada ya kuzunguka sana na vyeti vyangu kusaka ajira bila mafanikio,nimeamua kwa dhati kabisa kuwekeza kwenye kilimo,nimekuja hapa kuwaomba ushauri kwa wale wenye uzoefu,je ni kilimo gani kinafaa kufanyika kuati ya mwezi wa tatu katikati na mwezi wa nne?najua mahindi nitakua nimechelewa ila je ni kilimo cha mazao gani hata kama ya umuagiliaji (maana nimenunua machine ndogo ya kuvuta maji,na shamba halipo mbali na mto) yatafaa na yatatakiwa sokoni iwapo yatalimwa mwezi huo?nina shamba la heka mbili,nimenunua mkoani Morogoro,wilayani Kilosa!Mtaji wangu mpaka sasa ni shilingi laki nne (400,000/=) natanguliza shukrani kwenu wadau