Pole sana mkuu. Hii ni frustrating issue kwako. Kutokuwa na sperms zenye nguvu ya kuzalisha inasababishwa na mambo mengi kama magonjwa ya zinaa, ulevi, stress, lehemu nyingi mwilini, kutopumzika na mengineyo mengi ambayo bila shaka tabibu kakujuza.
Unaweza kuepuka tatizo hili kwa kuacha kunywa vinywaji vinavyoathiri male fertility kama Coca-Cola, Pepsi na vingine vya aina hiyo. Pia acha vyakula vyenye lehemu nyingi. Epuka machipsi nk. Kula vyakula vya nafaka visivyokobolewa, vyakula vya mizizi kama viazi, mihogo, karanga. Tumia virutubisho vya asili kama asali badala ya sukari. Kunywa maji ya kutosha. Fanya mazoezi mara kwa mara kuupa nguvu itakiwayo mzunguko wako wa damu. Lala muda wa kutosha angalau masaa saba hadi nane kwa siku. Punguza stress (najua haziepukiki). Furahia kufanya mapenzi. Epuka kuoga maji ya moto sana halafu kwa muda mrefu.
Nenda kacheki damu ama afya kwa ujumla ili kuona kama hali hiyo imechangiwa na magonjwa ya zinaa.
Tumia pia muda wako kujielimisha mtandaoni juu ya namna ya ku overcome male infertility.
Ninaamini utalishinda hilo tatizo na kumpiga mimba mwanamke.
Kabla sijasahau, mhimize pia mwenza wako apime UTI. Pia msisitize juu ya kuitunza afya ya kumani.