Ushauri: Nimefanyiwa sperm analysis ikagundulika siwezi kumpa m/mke ujauzito



Kwa nini unataka upate mtoto/watoto? Hii nchi imeshajaa hiyo ni habari njema kabisa kwanza ikitokea wanaume wengi kama wewe Mungu ashukuliwe, hakuna njia nyingine ya kupunguza watu!
 

Pole sana kaka. Mungu aliyeumba Mbingu na Dunia hujawahi kushindwa na Jambo lolote lile. Changamoto unayopitia ni kubwa na Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kukuvusha hapo. Ningependa kukushauri kuwa nunua kingamuzi chenye Emmanuel TV na uwe una angalia namna ambavyo watu wengine wenye matatizo ya aina hiyo wanatoa shuhuda kwa namna ya ajabu kabisa Mungu alivyowaponya na tatizo kama hilo na sasa wana watoto tena wenye afya tele. Imani yako itazidi kuongezeka kila siku.....Nawe Mungu atakuhudumia siku moja sawa sawa na kiwango cha Imani yako. Usife moyo....take courage....Fanyia Kazi na ushauri huu pia. Barikiwa
 
Mimi pia yamenikuta ila nimeanza dozi, hata hivyo nina mtoto mmoja ambaye nilipata kabla ya kuoa
Aisee, lakini nguvu za kiume unazo za kutosha? Tuwe makini na laptops, mipombe, baadhi ya dawa za hospital nk ni hatari sana kwa afya ya uzaz
 
Pole na kuwa na subra kwa tatizo hilo ila uckate tamaa na rehma ya Allah ....pili kama hutojal wasiliana nas tunazo Dawa za asili na kiarabu na KWA uwezo wa mwenyez zimewasaidia watu wawili(wanawake) na wamepata ujauzito baada ya kushindikana hospital ...so zipo Dawa kimuonekano ni za kawaida ila Allah amezipa nguvu .....wasiliana nas 0712770729
 
hiyo ogopa sana kuifanya ukiambiwa umeumbwa kutozaa na mkeo tayari keshakuzalia watoto 4 lazima utafute panga
 
Post yako haijamtendea haki mletamada...anyway, i hope Mungu hatakuadhibu kupitia watotowako.
Watu kama hawa ndio wakufungiwa imeniuma utafikiri mie ndio mhusika binadam tuna roho mbaya sanaa
 
Atakuwa mwanaume wa Dar huyu kazi kula viepe kila siku.
 
Pole sana ndugu kwa matatizo hayo, naamini utapona! Ushauri wangu ni kuwa; Kwanza kabisa hakikisha kuwa unapima na kuchunguza kama una magonjwa ya zinaa. Kuna magonjwa kama Kaswende huwa vigumu sana kuyagundua na waweza kupima vipimo vyake na isionekane. Ukishagundua huna maradhi yoyote basi kuna dawa zinazotibu kabisa, kikubwa kwanza ondoa stress uwe na amani na furaha. Kuna vituo vya afya vingi vinavyotibu tatizo hili. Waweza nitafuta pm nikuelekeze baadhi
 
janjab;pole sana ndugu,jaribu kwanza kipimo IVF,na hicho kipimo kinapatikana Nairobi tu,kwa hapa bongo sidhani kwa kweli,pale ndo unaweza kupata jibu is tatizo lako,
Mdau anahitaji matibabu sio kipimo, kwa mujibu wa maelezo yake ameshafanyiwa vipimo na sasa anahitaji matibabu ya tatizo lake
 
Subri kumegewa tu maana hakuna namna
Akili za kipumbavu na ukosefu wa hekima na ustaarabu zero, mbona mnageuza jf kuwa kijiwe cha vilaza!!? Mtu anatatizo wewe unaleta komenti zisizo na maana kibinadam, huna empathy wala sympathy, ur merely a wild hog!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…