pole ndugu, hawajakupa hata ushauri au njia ya matibabu? Pili ningekushaur uende kwa wataalam wengne uskie nao wanasemaje na wakupe solution pia, usiwe na shaka hakuna lisilo na ufumbuz. Mungu yu pamoja nawe.
Ni vigumu kupata ushauri mzuri kwa jinsi uzi wako ulivyouweka, inaonekana bado Daktari aliyekuona yuko katika hatua ya uchunguzi na hajagundua ni kipi kinachokusibu kati ya busha na mshipa ambavyo ni maradhi mawili tofauti yanayohitaji tiba tofauti.
Nakushauri urudi tena kwa Daktari wako aweze kukufafanulia vizuri kile alichokigundua na zaidi sana kukutoa wasi wasi kwa kuwa hayo maradhi mawili yanatibika kwa kufanya upasuaji mdogo tu.