tungejua uko wapi, namaanisha mkoa au hata wilaya, au una access na maeneo gani ingekuwa rahisi zaidi kukushauri kwani fursa zinatofautiana kulingana na mahali ulipo
lakini kama ndo kwanza umezipata, nakushauri uzitafutiea fixed account ya hata mwaka mmoja ili akili itulie kwanza, maana kiukweli ukipata hela kama hiyo bila kuwa na wazo au kutegemea, kwanza unaweweseka, na ukija kukaa sawa imebaki m10, hapo unapata frustration, ukija kujipanga zimekata na hapo ndo utakuwa maskini milele maana wansema opportunity never come twice
lakini kama uko dar, angalia biashara ambayo unaweza kuwa na uzoefu nayo, au unaweza kuimudu kwa muda mfupi, na usijaribu kuwaamini watu au mtu yeyote katika biashara, na usijaribu kumuagiza mtu sijui dubai, au china wala singapore itakula kwako mkubwa (nina wafahamu watu zaidi ya 7 ambao wameachwa njiani kwa kuagiza au kuamini watu kwa hela nyingi)
kwa sasa mkuu nakushauri uchukue m70 weka kabisa fixed account ya mwaka, na hiyo m10 tumia kufanya test za biashara, au kutafutia ujuzi wa biashara kama kuwaona wataalamu wa biashara, kufanya kozi fupi za ujasiriamali na kupata exposure ya biashara tofauti tofauti
Kama utakuwa tayari unaweza kuni PM pia naweza kukusaidia kwa njia moja au nyingine (ingawa kwa sasa sipo nchini - niko Uholanzi kwa masomo ya mda mfupi - narudi mwezi wa saba, na pia ni mwl wa masomo ya biahsara katika moja ya vyuo vikuu hapo bongo) so sitahitaji ujira, wala kujua hela yako ilipo wala taarifa zako za kibenki, uwe na amani kuwa utakuwa na mtu mpenda maendeleo.
Hongera pia kwa kupata mtaji mkuu, komaa uuzalishe maana bongo ni ngumu, na kwa kweli ni dunia nzima, maana hata huku si shwari sana