Nawatania
Senior Member
- Jul 13, 2021
- 148
- 549
Rushwa ya ngono imekuwa janga kwenye nchi yetu kuanzia Shuleni, Vyuoni na Kazini.
Je tunafanya nini kudhibiti rushwa ya ngono na mahusiano?
I:SHULENI
Nafikiri kila sehemu janga hili linatofautiana na sehemu nyingine kulingana na mazingira.
Shule zinaathiriwa sana na mahusiano ya walimu na wanafunzi, ngono zembe kati ya watoto wa kike na kiume shuleni,watoto wa kike na boda boda, watoto wa kike na vinyozi na watoto wa kike na madereva hawa ndio wanachukua asilimia kubwa ingawa kuna watu wa kada zingine mtaani.
Lakini vile vile kuna mahusiano ya ngono kwa watoto wa kiume na walimu wa kike, watoto wa kiume na wamama mtaani, watoto wa kiume na wadada mtaani.
Nini kifanyike?
Ukifanya uchunguzi sana utagundua katika shule za msingi na sekondari watoto ufanya ngono kwa sababu ya kutaka kujaribu kwa wanayoyasikia kwa wengie, pili ufanya ngono kwa ushawishi wa kupewa vitu vidogo vidogo na tatu tamaa.
Pia ukifanya utafiti kwa shule nyingi za msingi na sekondari ambazo wakuu wake ni wa kike mahusiano yapo chini sana ukilinganisha ambazo zinaongozwa na wanaume naruhusu kupingwa maana ni utafiti huru.
Sasa kulingana na hoja hizo naomba kutoa njia zitakazotumia kupunguza au ikiwezekana kuondoa kabisa tatizo la ngono na mahusiano maeneo ya shule.
1: Wizara ya elimu itangeneze sheria na miongozo wanafunzi wa kike watembee wawili wawili wawapo na sare za shule.Shuleni, nyumbani na mtaani iwe ni marufuku kutembea mwenyewe hata akiitwa ofisini na mwalimu hata akiwa unaenda chooni lazima wawe watoto wawili wa kike pia wakiume wawe wawili.
2: Wizara ya elimu kwa kushirikiana na Wizara ya afya waanzishe program ya kupima HIV na mimba Mara kwa mara hata kwa kushutukiza mashuleni kwa kuchagua baadhi ya wanafunzi kwa kuwatumia walimu ingawa majibu ya HIV yawe siri kati ya shule na mzazi.
3: Kuwepo kwa udhibiti wa utoro mara kwa mara ili wanafunzi wasiwe wanazagaa mtaani.
4: Kuwepo kwa ratiba ngumu shuleni na homework nyingi zitakazomfanya mwanafunzi awe na kazi nyingi za kufanya awapo nje ya shule (nyumbani) hii itapunguza uzululaji kwa watoto wa kutwa na pia kazi nyingi kwa watoto wa bweni.
5: Kuendelea kuongeza walimu wa kike wengi mashuleni na kuwapandisha vyeo angalau wawepo kwenye watu wawili wa juu wanaotoa maamuzi katika shule husika hii itasaidia kufatilia kwa ufasaha mienendo ya watoto hasa wa kike kuwapa semina za malezi kuwaondoa katika hatari ya mahusiano.
6: Takukuru pia watoe semina kwa watoto za mara kwa mara kwamba ni wapi pa kwenda kushitaki ikiwa mtu mzima anamlazimisha mtoto kufanya naye ngono.
7: Zianzishwe au zitengwe shule maalumu kwa ajili ya watoto mcharuko wa kike na ziwe chini ya walimu wa kike waliosomea saikolojia hivo mwanafunzi akishindikana katika shule moja ili asiwaharibu na wengine anaondolewa kama kafukuzwa ila anapelekwa shule ya mbali. Lakini shule husika ishirikiane na mzazi husika.
II: RUSHWA YA NGONO CHUONI
Hapa ndipo kuna hatari kubwa ya maambukizi ya virusi ya Ukimwi, watoto wengi wanajiachia sana wanapofika chuo ila sio kosa lao ni kosa la sayansi na tekinolojia lakini pamoja na hayo tusichoke tunaweza kudhibiti rushwa ya ngono vyuoni.
Chanzo kikubwa kinachosababisha rushwa ya ngono vyuoni ni mitihani sasa tunafanya nini kudhibiti?
1: Mitihani yote inayofanyika vyuoni kama ni vyuo vya Serikali wafanye kubadilishana mfano mitihani ya chuo kikuu Dar es Salaam ikasahihishwe chuo kikuu Dodoma na ya Dodoma iletwe Dar es salaam hivyo hivyo hata kwa vyuo vya private wabadilishane .hii sio kwamba itapunguza rushwa ya ngono pia itapunguza elimu bandia ambazo hazina uhalisia wa kimaisha na walichosomea mara tu watoto wanapomaliza elimu ya juu.
2: Ufungaji wa kamera za CCTV katika maeneo ya vyuo na watoto wa kike kutembea wawili wawili wawapo maeneo yote ya chuo maana kuna wakufunzi wengine uwa wanashawishi watoto wa kike wakiwa ofisini hii itasaidia kupunguza watoto wa kike kuombwa rushwa ya ngono wawapo ofisini kwa wakufunzi kufatilia mambo yao mbali mbali.
3: Kuwepo kwa maafisa wa takukuru wanafunzi katika vyuo mbali mbali ambao kazi yao kubwa ni kukusanya taarifa za rushwa ya ngono na kuweka mitego mbali mbali katika maeneo yao ya chuo wanachosoma pia kutumia tekinolojia ya mawasiliano kufatilia baadhi ya watu ambao wanashukiwa kuomba rushwa ya ngono kwa kutumia Simu na komyuta na vifaa vingine kuwanasa na ushahidi.
4: Wazazi kuwaandalia watoto pesa za kwenda kusoma chuo wakiwa bado shule za kawaida hii itapunguza tamaa ya kufanya mambo ya hatari chuoni maana mtoto akipata mkopo pia akiwa na pesa kutoka kwa mzazi za kutosha kutamfanya asifanye mambo ya hatari katika maisha yake pale chuo kama kujiuza na kuingia kwenye vishawishi vya kuombwa rushwa ya ngono.
5 : Mwisho Wizara ya elimu, Wizara ya afya na NGO's kuendelea kutoa elimu na kupima afya na kuhamasisha kutumia kondomu kwa watoto wa kike na kiume wawapo vyuoni na nje ya vyuo maana maradhi bado yapo.
III:RUSHWA YA NGONO KAZINI
Hapa ndio kuna hatari zaidi kumekuwa na rushwa ambayo imepitiliza, kwanza ni wale watoto wa kike wanataka kupata kazi, pili ni wale walipo kazini wanalinda vyeo vyao kuendelea kuwepo na tatu ni wale waliopo kazini wanataka kupanda vyeo.
Hapa nashauri yafuatayo
1: Serikali waangalie kwa makini maafisa wake kwenye halimashauri na idara zake maana huko ndio madudu yamejaa.
Tuimalishe tekinolojia ya mambo yote ya wafanyakazi wanayohitaji kama uhamisho, kupanda cheo, kufatilia sitahiki za wafanyakazi yaani kila huduma unayohitaji kama mfanyakazi ipatikane kwenye mtandao na upate majibu kwenye mtandao kwa mfanyakazi kuingiza taarifa zake.hii itapunguza yale mambo ya njoo kesho, tukutane kwenye baa fulani, njoo na document fulani kumbe kama ni mwanamke anazungushwa ili atoe rushwa ya ngono.
2: Upande wa makampuni na taasisi binafsi wajitahidi kuwa na waajiri wawili wa kike na kiume ili pia kuhepusha mambo ya kuingiza watu wasio na sifa kwa sababu ya ushawishi wa nje na fani na uwezo wa anayehitajika
3: Takukuru iwe na maafisa wake wa kike warembo ambao inawapeleka kama mtego kuomba kazi husika kwenye taasisi za Serikali na binafsi(Makampuni) hii itachangia kupunguza rushwa ya ngono kabisa makazini.
Tukifanya haya naamini tutamaliza au kupunguza kwa asilimia kubwa rushwa ya ngono Chuoni na Kazini na mahusiano Shuleni.
Nashukuru kwa muda wenu naomba kuwasilisha kama kuna watu nimewakwaza naomba tusamehane mimi ni binadamu.

Upvote
2