ushauri please!

ushauri please!

mamkindi

Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
61
Reaction score
5
Nina tatizo la kutokuwa na mzunguko wa hedhi ambao ni regular, kuna wakati unakuwa baada ya siku 26, 27,28,29,30,na 33 kwa kifupi naweza kuwa na mzunguko mfupi au mrefu na hauna mpangililio. kwa sasa nimefikilia hatua ya kutaka kupata mtoto, nishaurini wanaJF nifanyeje au ni siku zipi naweza kupata ujauzito
 
wataalamu wanakuja dada watakushauri
 
Nakushauri kamuone Gynaecologist!! Huu wa bure uwe kama supplimetary
 
Weka tarehe zenyewe hapa jamvini ili wataalam na ma dr wajiridhishe wakati wanatoa ushauri. Unawezakuwa uhesabuji wako labda una hitilafu,ila wataalam wanakuja na hatimaye mambo yatakuwa sawa.
 
Kuanzia siku yakumi toka uanze siku zako unaweza kupata ujauzito
 
Gynae=Daktari Bingwa wa masuala ya uzazi kwa wanawake
 
jamani Mamkindi wewe! Ukishasikia daktari Bingwa si unakwenda Hospitali yoyote kubwa ya mkoa au private hospitalunaulizia Gynae? haya basi, Nenda Mikocheni Kairuki Hospital utamkuta Dr Clementina. Sasa utaniambia sipo Dar au sina hela ya kulipa!!
 
kama siku zako haziendi vizuri unaweza kuhesabu kuanzia siku ya 11 tangu umeanza hedhi ya mwisho mapaka siku ya 16 angalau ni tarehe nzuri za kupata mtoto. Na unashauriwa kukutana na mwenzio at least after every 48 hours. Si kila siku, kuna sababu za kitaalamu.
 
Mzunguko wa hedhi ni siku ya 1 ya hedhi mpaka siku ya 1 ya hedhi nyingine.Ingawa wastani wa mzunguko ni siku 28,ni kawaida kuwa na mzunguko mfupi au mrefu.

Muone Daktari kama unamabadiliko makubwa katika mzunguko wako wa hedhi,na hasa kama una mizunguko 3 au zaid inayochukua siku zaid ya saba ukiwa kwenye hedhi.

pia ni vizuri kumuona Dr. kama una bleed katakati ya period au una maumivu ya nyonga nje ya mzunguko wako.
 
Back
Top Bottom