Ushauri plz! Umefanya usaili then unaambiwa utoe hela ndo upewe ajira!

Ushauri plz! Umefanya usaili then unaambiwa utoe hela ndo upewe ajira!

ndyoko

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,971
Reaction score
1,652
Kuna jamaa yangu alifanya usaili, sasa jana
kaambiwa na mtu anayedai anafanya kazi kwa hiyo
ofisi kwamba inabidi atoe hela kwanza ili aweze
kupewa hiyo ajira. Huyo mtu inaonekana amepata details
za kwenye CV ya mhusika kwani alikuwa anajaribu
kusoma maelezo binafsi ya mwajiriwa mtarajiwa.

Jamaa bado hajaamua kama atoe au laaa, maana
kazi anaipenda lakini hana uhakika kama akitoa hiyo
hela kweli ataipata hiyo kazi au ndo itakuwa imekula kwake.

Mshaurini huyu ndugu please!
 
Mbona rahisi.....jamaa amwambie siku ile atakaposaini mkataba tu....akitoka hapo anamtoa........akitoa kabla imekula kwake....akishaingia kazi hata asitoe hiyo hela!!
 
Amwambie kwamba akishaajiriwa mshaara wa kwanza atapiga pasu nae so ampitishe kwanza
 
Mbona rahisi.....jamaa amwambie siku ile atakaposaini mkataba tu....akitoka hapo anamtoa........akitoa kabla imekula kwake....akishaingia kazi hata asitoe hiyo hela!!

Ndivyo great thinkes tunavyotakiwa kufikiria. Mwambie asitoe pesa. Ushauri wa huyu mdau ndio anaotakiwa kuzingatia.
 
Back
Top Bottom