Ushauri: Rais Samia Suluhu Hassan iga mfano wa Angela Merkel

Ushauri: Rais Samia Suluhu Hassan iga mfano wa Angela Merkel

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Mama Rais anayengojea kuapishwa. Kwanza salamu. Tanzania inakujua na kukuamini tokana na uchapakazi na uzalendo wako. Hata hivyo, una kazi kubwa kuvaa viatu vikubwa vya marehemu Magufuli. Si haba.

Unaweka historia kwa mara ya pili. Mara ya kwanza ulichaguliwa makamu wa kwanza mwanamke nchini.

Sasa utaapishwa kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini na makamu na rais wa kwanza mwanamke toka visiwani.

Una kazi kubwa na nzito hasa wakati huu ambapo taifa limo kwenye msiba mzito. Hata hivyo, unao uwezo na uozefu si haba.

Leo sisemi mengi bali kukutaka ujifunze sana toka kwa Chancellor wa Ujerumani anayeondoka Angela Merkel.

Jifunze yafuatayo kuhusiana na uadilifu na utendaji:

Mosi, usiruhusu ofisi yako kuwa mali ya ukoo wala ndugu na jamaa.

Pili, chapa kazi bila kutaka makuu huku ukizingatia kuwa kuna maisha baada ya urais.

Tatu, uwe muadilifu wewe na waliokuzunguka.

Nne, uwe mwingi wa vitendo na mchache wa maneno.

Tano, epuka umaarufu wa kupigwa picha kila mara.

Sita, endelea kumkinga mumeo toka kwenye siasa na nafasi yako.

Saba, rekebisha mapungufu yoyote aliyoacha bosi wako ambayo unayajua.

Nane, muenzi mtangulizi wako kama alivyofanya Merkel.

Mwisho, epuka siasa za uchama, ukanda, ubara na upwani, ujinsia, ubabe na badala yake ufanye siasa za utaifa.

Kwa leo haya yanatosha.
 
Ujumbe mzuri ila hujazingatia style ya uandishi, weka paragraph katika ujumbe wako.
 
Mwenzake anaongoza taifa la wastaarabu, watu waliostaarabika mkuu. Unataka aibebe Tanzania na watanzania kistaarabu? Hembu acheni masihara nyie. Aiongoze Tanzania kama Merkel anavyoingoza Ujerumani?

Watu ndani ya siku kadhaa washachapa nearly 200b waongozwe kistaarabu? Nchi ngumu hii...
 
Uko sahihi, watu wabishi wabishi sana. Kila mmoja anataka atimiziwe anayoyataka yeye.
 
Back
Top Bottom