Man from cuba
JF-Expert Member
- May 2, 2021
- 571
- 1,394
Waziri mpya wa TAMISEMI na Waziri mpya wa Elimu wanatakiwa kulichukulia kwa uzito suala la walimu wanaofundisha vijijini kwa kuwapa motisha mbalimbali ili maombi ya uhamisho wa walimu ipungue.
Imekuwa mtihani mkubwa kwa watumishi hawa wa elimu kukaa vijijini ambako huduma hazipatikani,changamoto ya usafiri,ushirikina etc.
Walimu wengi wamekuwa wakipambana kwa njia yoyote kuhama hadi waziri wa TAMISEMI aliyekuwepo kusitisha uhamisho lakini tukija kwenye uhalisia hakuna mtumishi anayependa kubaki kwenye mazingira mabaya kama hayo.
Nimemsikia mbunge wa Makete akilalamika ukosefu wa Waalimu wa kike jimboni kwake kitu kinachowapa ugumu wanafunzi wa kike hasa wanapovunja ungo, lakini ukiliangalia kwa undani suala hilo sio kweli kwamba serikali haipeleki walimu huko lakini wote wanahama hasa walimu wanawake hivyo serikali ingeanzisha posho na hardship allowances kwa walimu wanaofundisha vijijini ili angalau kuwatofautisha na wa mijini.
Serikali ikifanya hivyo pamoja na upungufu mkubwa wa walimu ukilinganisha na idadi ya wanafunzi angalau itakuwa imetibu changamoto ya upungufu wa walimu wa kike vijijini tofauti na hapo yatakuwa kama ya kata moja kigoma ambayo ina mwalimu mmoja tu wa kike kata nzima.