Ushauri: Serikali Ianzishe Ofisi Ya Kutoa Elimu Ya Biashara na Kuhamasisha Ujasiriamal

Bw.Daffa

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
420
Reaction score
116
WanaJf.

Swala la ajira limekua ni changamoto kubwa sana.Na mbaya zaidi ni kwamba hata vijana wakiamua kujiajiri bado wanakumbana na changamoto mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine zinatokana na kukosa Elimu ya Kuendesha Biashara.Ripoti Iliyotolewa na World Bank Group Tanzania inataja waziwazi kwamba Wafanyabiashara Wadogo Wadogo Wengi Tanzanaia Wanafocus Kwenye Kuhakikisha Kwamba Bisiness startups Zao Zinasurvive na Wala Sio Kukua.Na Nyingi Huishia Kufa Ndani ya Miaka Mitano..

Wakuu Mtakubaliana na Mimi Kwamba Ili Kuendesha Biashara Flani Kwa Mafanikio Itabidi Mhusika Awe na Atleast ABCs za Biashara.Na Ndo Mana Leo Hii Kuna Utitiri wa Business Consultant Firms.

Ila Mimi Niliwaza Kwa Upande Wa Serikali.Kwamba Serikali Ianzishe Ofisi Kila Wilaya za Kutoa Elimu ya Biashara na Kuhamasisha Ujasiriamali.. Vitu Vidogo Vidogo Kama Namna ya Kuandika Business Plans,Tax Management,Business Leadership n.k Ambavyo Vitainua Biashara Nyingi Ndogo Ndogo na Hivyo Kuongeza Nafasi za Ajira.

Kwa Serikali ya Marekani Wanafanya Hii Kitu Kupitia Us Small Business Administration.Na Ipo Pia Tovuti Ambapo Kuna Tutorials na Artocles Nyingi Zinazotoa Elimu ya Biashara.
Tembelea Us Small Business Administration Utajionea.
Kwa Hiyo Hata Kwa Serikali Yetu Pia Ikiwa na Website Maalum Kama Hiyo Itakua ni Nzuri.

Kuna Haja Kubwa Kwa Serikali Yetu Kuchukua Hatua Zinagusa Moja Kwa Moja Vijana Wakitanzania Mbali na Kuvutia Wawekezaji tu Ambao Mda Mwingine Huja na Wataalam Wao.

Mnainaje Huu Ushauri Wakuu..!Kuna Ugumu wa Kufanya Kitu Kama Hiki.
 
Serikali imeteuwa Jiji la Dar es Salaam kuwa kituo maalum.

Wewe kama upo mkoani njoo jiji la Dar upate Shahada yajo ya maisha

Wale wote uliokuwa ukiwaona mabwege Mkoani leo hii ndio wanakimbiza Jiji kwa maisha mazuri.
Humjui mwenye Elim wala asie na Elim,karibu sana Dar es Salaam City University
 
Ofisi zipo sema walioko huko hawajui wajibu wao. Kuna kituo cha uwekezaji TIC hizo ndo kazi zao. Wao wana focus kwa wawekezaji wa nje tu.

Kuna baraza la taifa la uwezeshaji kiuchumi, kuna wizara nzima ya viwanda na biashara. Nikuulize tu unafikiri maafisa pale viwanda na biashara kila wakiamka na kwenda ofisini wanafanya kazi gani.

Kuna brela, wao kila kukicha wana sajili biashara tu lakini hata siku moja hawasumbuki kuangalia ke biashara wanazo sajili zina endeleaje?

Kuna TRA wao hata kabla ya kuanza biashara wanakulipisha kodi halafu wanakuacha bila elimu yoyote ya kodi na wanategemea uende uingize fedha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…