Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Ukweli ni kwamba, japo bei ya mafuta mwezi huu imetangwaza kushuka, bado wananchi hawataona tofauti ya maana katika bidhaa na wala hakuna uhakika kuwa huko mbeleni mafuta yataendelea kushuka kwani yanaweza kupanda pia.
Hivyo, kwakuwa bei ya bidhaa na huduma kwa kiasi kikubwa inachangiwa na bei ya mafuta(gharama za usafirishaji), nashauri serikali iharakishe matumizi ya gesi ya asilia kwenye magari kwani itachangia kupunguza gharama za usafirishaji.
Tukianza kutumia teknolojia hii kwenye magari, moja ya madhara inaweza kuwa ni serikali kukosa kodi inayotokana na uagiza na uuzaji wa mafuta(kodi husika kupungua). Hata hivyo, ni wazi pia tutaimairisha shilingi yetu dhidi ya dola kwa kupunguza kiasi kikubwa cha hela za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta nje.
Hivyo, ni jukumu la serikali kuamua kusuka au kunyoa. Bei ya gesi haiwezi kulingana na bei ya mafuta na hivyo gesi italeta tofauti na mapinduzi makubwa kiuchumi katika nchi yetu tukiwa na sera nzuri kwenye hii sekta ya gesi.
Kwa kuanza, serikali inawezekana kutoa incentives kama punguzo la kodi kwenye kuingiza facilities zitazotumika kukamilisha matumizi ya hii teknolojia na mambo mengine ya aina hiyo.
Hata hivyo, sitashangaa kuona wenye interest kwenye biashara ya mafuta wakawa kikwazo kwa namna moja au nyingine.