Taasisi nyingi za Serikali hazimjali Mteja. Zina huduma mbovu na ikitokea Mteja ndiye umekiuka taratibu zao (ambazo nyingi hata elimu hawatoi na hazijulikani) wanakuumiza na faini na adhabu zisizohimilika...
Mfano mwingine ni TBS wanalazimisha wafanyabiashara wajisajili online lakini kuna mlolongo mrefu sana usioeleweka kwenye kujisajili. Muda mwingi mtandao unasumbua, Na lugha ni moja tu, Kingereza..
Wengine ni Wakala Wa Vipimo, wanakukamata mfanyabiashara kwa kutumia Mizani Mpya usiohakikiwa wanaacha kuwabana waingizaji na wauzaji wahakiki Mizani yao kabla ya kumuuzia Mteja.
TRA nao kila siku mtandao unasumbua, mpaka mtu unajiuliza why wasisitishe Mkataba na huyo inconsistent Network provider?
Awamu hii ya Utawala Taasisi nyingi za Serikali zinafanya kazi kwa kuvizia Wateja, ili waongeze mapato. Na siyo kwa lengo la kuboresha huduma.