Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Nashauri serikali ije na mikakati ya muda mfupi wa kudhibiti ugonjwa huu na mkakati mmojawapo uwe ni kutoa chochote(fedha,cheti maalumu,n.k) kwa yeyote atakaepimwa na kugundulika na corona na kisha akaamua kujitangaza mwenyewe hadharani au akaruhusu atangazawe hadharani na mamlaka husika na picha zake kusambazwa kwenye vyombo vya habari.
Kwa mfano,serikali inaweza kuwapa vyeti maalumu vya kutambua mchango wao katika mapambano dhidi ya corona, na watu hawa wanaweza pia kupewa kipaumbele na serikali katika maswala mbalimbali kama vile utoaji wa ajira kwa walio na sifa,kupewa mialiko katika matukio yoyote yanayohusiana na ugonjwa huu,n.k.
Moja ya faida ya kufanya hivi,ni kuwa,mbali na kupambana na ugonjwa huu,pia itasaidia sana kupunguza kama sio kuondoa kabisa unyanyapa dhidi ya wote watakaothibitika kuugua ugonjwa huu ambao ni ugonjwa tu kama magonjwa mengineyo.
Hata hivyo.hatua hii itakuwa na maana katika kipindi hiki ambacho wagonjwa ni wachache kwani wagonjwa wakiwa wengi sana, inaweza ikapoteza maana.
Hivyo,kwakuwa hatujaamua kuthibiti mikusanyiko kama wenzetu huku wagonjwa wakiwa bado ni wachache,nadhani huu ndio wakati muafaka wa kutumia mbinu kama hizi ingawa kuna wachache wanaweza kuzitumia vibaya fursa za aina hii.
Kuwajua wagonjwa tofauti na kuwasikia(hata kama watakuwa wamewekwa kwenye karantini), kuna impact kubwa sana hasa kwa wanaodharau huu ugonjwa wakiamini wao ni vijana,n.k.
Watu hawa pia wanaweza kutumika kama mabalozi katika mapambano dhidi ya corona ikiwemo kuhamasisha michango pamoja na mambo mengineyo yanayohusiana na ugonjwa huu.
Ni ushauri tu.