Nilienda Bagamoyo Kidomole kuangalia shamba langu. Wakati nasubiri wafanyakazi wangu waje njia panda nikaona gari lina park na wachina wawili wakashuka wakaenda kwenye kibanda na kurudi na mfuko.
Nilishangaa kuona wachina wako huko. Nilivyo uliza watu wa pale wakasema ni wamiliki wa machine za kamari na pesa nyingi za bodaboda zinaishia huko. Cha ajabu ni kwamba wachina wanapita kukusanya pesa sio kuweka pesa!.
Hii ni biashara ambayo haina faida yoyote na hiyo kodi wanayopata serikali ni ndogo ukilinganisha na pesa zinazotoka kwenye hizi jamii masikini.
Mfanyakazi wangu alienda kuweka reheni pikipiki yangu ya laki tisa kwa laki moja na nusu ili wampe pesa za kamari.
Ushauri wangu ni kwa serikali kusitisha kamari zote ambazo hazihusu wageni. Yaani kamari zibaki kwenye hotel za wageni wa nje maana hizo pesa zinakuja nchini lakini kamari kwenye vijiji na mijini zisitishwe mapema.
Kamari hazisaidii llolote kwa watu wala serikali. kamari haziongezi pato la taifa, haziongezi ujuzi, hazileti kazi wala uwekezaji. Serikali fanyeni hili mapema sana