Kwa muda sasa tangu serikali ya awamu ya Tano ilipoingia madarakani, kumekuwa matumizi ya lugha ambayo inaakisi uelewa mdogo wa diplomasia ya kimataifa na diplomasia ya kiuchumi ukilingamisha na utawala wa Mzee Jakaya.
Viongozi mbalimbali wa chama na serikali wamekuwa wakitumia maneno yasiyofaa kidiplomasia kama vile "BEBERU" kurefer mataifa wahisani, mashirika ya kimataifa na mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi.
Lazima tutambua sisi ni taifa Lenye nguvu ndogo sana kiuchumi duniani, uchumi ambao maelfu ya vijana hawana kazi, uchumi ambao miradi ya maendeleo tunategemea wahisani. Uchumi ambao hatuwezi ongeza mishahara, uchumi ambao hatuwezi lipa deni la ndani etc.
Lugha zinazotumiwa na wanasiasa kuonyesha kwamba tuna vita ya kiuchumi na mataifa makubwa tutaishia kupoteza. Na tukipoteza huo uzalendo hautoonekana.
Suala la watoto wa kike kupata mimba halikuanza leo, hii sheria ilikuwepo toka zamani. TATIZO KUBWA NI VIONGOZI KUONGEA MAJUKWAANI KWA MBWEMBWE HUKU TUKIPELEKA MKONO KUOMBA. Mbona Mzee Kikwete alilinyamazia? Mkapa alinyamaza? Kwanini uende kuongea majukwaani?
Viongozi pimeni kauli zenu, Watanzania wakibanwa na hawa wakubwa wa dunia tutageukiana sisi kwa sisi. Maendeleo ya dunia ya sasa yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mchango wa wawekezaji kutoka nje ya nchi. Tujifunze kuongea kwa hekima.
Leo nimesoma tweet ya Mwigulu akitumia Maneno "MABWANA ZAKO" hii yote ni kukosa hekima. Hao mabwana ndio wanashikilia uchumi wa dunia hii. Na ndio hao wametunyima Dola mil 500. Wakituamulia hamna atakae baki salama.
HEKIMA! HEKIMA! HEKIMA!!