Ushauri: Shirika la reli (TRC) uzeni vyuma na mitambo chakavu kwa viwanda vya vyuma vya ndani maana hamna matumizi navyo

Ushauri: Shirika la reli (TRC) uzeni vyuma na mitambo chakavu kwa viwanda vya vyuma vya ndani maana hamna matumizi navyo

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
4,035
Reaction score
11,462
Ushauri huu nautoa mara ya pili baada ya kuzungumzia suala hili miaka kama 3 huku nyuma.

Kikawaida mali za Shirika la uma kama TRC zimekuwa zikitunzwa kwa ufanisi mkubwa na kati ya mashirika yaliyofanikisha pakubwa kuzuia wizi na upotevu wa vifaa, mitambo na vipuli basi ni Shirika la reli.

Pia sona: TRC yatangaza ratiba mpya ya SGR, Treni ya Express Dar-Moro haitasimama vituo vya njiani

Ombi langu kwa mamlaka Husika kwa kuwa tunazosheria za utunzajia wa mazingira ni vyema mitambo hii ya Shirika iliyozagaa nchi nzima ni bora ikauzwa kwa wenye viwanda vya chuma nchini ili malighafi hiyo itumike kuzalisha bidhaa mpya zitakazo chochea maendeleo ya kiuchumi.

Karibu maeneo yote ya vituo vya treni kuanzia Dar es salaam, Dodoma, Tabora, Mwanza na Kigoma Kuna kiasi kikubwa sana cha vyuma chakavu ambacho iwapo kitatumika ipasavyo kinaweza kuchochea ukuaji mkubwa wa uchumi.

Hivyo basi Shirika la reli @Tanzaniarailwayscorp pamoja na serikali angalieni namna ya kuviondoa hivyo vyuma chakavu ili vifanyiwe recycling kwa ajili ya matumizi mengine.

Wakusoma 12
 
Hili wazo sio kabisa wakiuza vyuma chakavu itachochea watu wengine kuhujumu miondombinu ya reli.
 
Hili wazo sio kabisa wakiuza vyuma chakavu itachochea watu wengine kuhujumu miondombinu ya reli.
Mbona wanyamapori tunauza na watu hawahujumu, ni authorized company tu ndiyo itanunua mkuu.
 
Sasa mavyuma chakavu Yale yanafanya Nini kwenye Shirika?
 
Back
Top Bottom