USHAURI: Simon Msuva nenda Simba ukainue kipaji chako, uwezo wako umeporomoka sana kwa kukosa mechi za ushindani

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Kiukweli kwa namna Simon Msuva anavyocheza sasa hivi, hakuna tofauti na wachezaji wengine wa ligi yetu ya NBC, tofauti na alipokuwa Wydad, Msuva hana stamina, hana confidence, hana control, anakata moto mapema sana, yote hayo yamesababishwa na kukaa nje kwa muda mrefu wakati akingojea hatma yake FIFA.

Namshauri Msuva, aende Simba tu kwani Yanga kumejaa na hawezi kucheza dakika 90, Simba atacheza hadi miguu ing'oke, otherwise Msuva anakwenda kupotea muda si mrefu.
 
Hapa ndipo unapoona kuwa makocha sasa wamekuwa mawakala
Hata wasio na namba asiwaite, makocha was timu za taiga huwa wanawaambia wazi nyota wao kama wanakaa benchi ama watafute timu wacheze la sivyo wasahau timu ya taifa lakini sisi huku tunawapa nafasi hata kama wanakaa bench
 
Kaka huyu jana alodhihirisha kuwa ni wa mchongo maana kocha mwenye weledi hawezi fanya maamuzi ya kipuuzi kama yale.

Na nina kwambia ita mgharimu sana maana tayari wachezaji wengine wataona kumbe kocha ana watu wake. Sasa unadhani mpole akiitwa next time atakuja na morali...sii anona ujinga tuu huu.
 
Sasa akienda simba ya akina Mugalu, Kegere, Bocco, Kibunenga! Siyo ndiyo kipaji kitakwisha kabisa! Yaani timu msimu mzimu inapata kombe la Bonanza, la Mapinduzi pekee!

Bora hata angeenda Coastal Union, timu iliyo fanikiwa kufika fainali Kombe la Shirikisho! Ila siyo simba bhana.

Ukiangalia hata kwenye mechi ya jana, Zimbwe ndiyo alikuwa uchochoro kwa Waaljeria, ukimlinganisha na beki 'katili' namba 2, Kibwana Shomari.
 
Kurudi kucheza nchini tena na umri unaenda ni gundu tu huku hakuna mpira, sitarajii msuva atatamani kucheza nchini tena labda Kama hana njaa au umri tatizo.
 
Namshauri Msuva, aende Simba

Upumbavu mkubwa sana badala umshauri akatafuta team nje wewe unataka abaki hapa hapa
Siyo upumbavu bali amemshauri kwa nia njema alinde kipaji chake wakati anasubiri shauri lake kutoka FIFA.
 
Sasa akienda simba ya akina Mugalu, Kegere, Bocco, Kibunenga! Siyo ndiyo kipaji kitakwisha kabisa! Yaani timu msimu mzimu inapata kombe la Bonanza, la Mapinduzi pekee!

Bora hata angeenda Coastal Union, timu iliyo fanikiwa kufika fainali Kombe la Shirikisho! Ila siyo simba bhana.

Ukiangalia hata kwenye mechi ya jana, Zimbwe ndiyo alikuwa uchochoro kwa Waaljeria, ukimlinganisha na beki 'katili' namba 2, Kibwana Shomari.
Simba ni ya 14 Africa. Wengine wajitaje wenyewe 😁😁 😁
 
Hata wasio na namba asiwaite, makocha was timu za taiga huwa wanawaambia wazi nyota wao kama wanakaa benchi ama watafute timu wacheze la sivyo wasahau timu ya taifa lakini sisi huku tunawapa nafasi hata kama wanakaa bench
Kukaa benchi inategemea mkuu mfano Bouna Sarr anasugua pale Bayern lakini ni panga pangua akiwa Senegal
Au wakati Xherdan Shakir yupo liver hakuwa na uhakika wa namba ila alikuwa mchezaji tegemeo wa Switzerland
 
Hapo kwa sarr umesema kweli jamaa akiwa Senegal anakiwasha vile vile ila huko anasugua benchi.
 
Kutopta nafasi ni tofauti na kukosa timu, mchezaj wa aina Hyo anafanya mazoezi kila siku na timu yake na maelekezo ya kocha anayapta. Sasa msuva anafanya mazoezi wapi
 
Back
Top Bottom