Ushauri sumu bora ya kupalilia mahindi na kunde kwa pamoja

Ushauri sumu bora ya kupalilia mahindi na kunde kwa pamoja

MUSHEKY

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
2,812
Reaction score
2,760
Kama inavyosomeka hapo juu wadau, nimelima mazao ya mahindi nikachanganya na kunde.

Changamoto niliyonayo nimechelewa kupalilia kwa jembe la mkono nataka nitumie dawa au "sumu" kupalilia

Shida ninayokutana nayo maduka nilipo ni kwamba wengi wanafahamu sumu za kupalilia zao moja pekee mfano mahindi peke yake au kunde pekeyake Si VYOTE KWA PAMOJA na kwamba iwapo nitazitumia kwenye mazao haya mawili niliyoyapanda pamoja basi zao moja litakufa

Kwa mwenye kuifahamu sumu inayofanya kazi kwa pamoja kwenye kupalilia mahindi na kunde anijulishe tafadhali
 
Muje wadau mnishauri hali tete
 
Sumu zilizopo ndivyo ulivyoambiwa hakuna namna.
Kuna zinazoua dicotyledon na zingine monocotyledon.

Amua kuua zao moja
 
Kwa kweli hiyo ni changamoto Mkuu, nami nilikumbana na kadhia hiyo mwaka huu mwanzoni...kila duka la pembejeo nililoulizia dawa ya kuua magugu katika shamba lenye Mahindi na maharage nilikosa. Nilichokifanya nilivunja bei nilipalilia kwa bei ya juu kuliko watu walionizunguka, namshukuru Mungu niliweza kukomboa mazao yote mawili.
 
Kupata selective herbicides kwa intercropping au mixed cropping ni ngumu sana bora uanze ndogo mdogo tu

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
tumia elimu ndogo ya darasa la sita juu ya
Monocotyledon na
Dicotyledon,wala usiumize muda kulizia hiyo herbicides kwani HAKUNA ICHO KITU DUNIANI
 
Back
Top Bottom