Kwa kweli hiyo ni changamoto Mkuu, nami nilikumbana na kadhia hiyo mwaka huu mwanzoni...kila duka la pembejeo nililoulizia dawa ya kuua magugu katika shamba lenye Mahindi na maharage nilikosa. Nilichokifanya nilivunja bei nilipalilia kwa bei ya juu kuliko watu walionizunguka, namshukuru Mungu niliweza kukomboa mazao yote mawili.