Wadau samahanini kwa kuingilia mada ya mtu mwingine...
Nilipenda kufahamu kati ya Swift na IST ipo ni nzuri kwa mishe za hapa mjini na kutoka kidogo nje ya mji
Swift ipo powa zaidi na kwa sasa spea zinapatikana sana. Tatizo la Vits au Ist zipo chini sana ukipata safar za barabara zisizo na lami au zenye mashimo ni shida sana. Lakin pia Swift hata ukikimbia speed 140 inakuwa stable zaidi.
Na pia ni kwasababu umetaja aina mbili za gar unataka moja wapo ila kwa mm nakushaur sana kama wewe ni kijana mwenye kipato cha kawaida kama mm ununue Noah, raha ya noah hulali njaa hata siku moja na kama una muda wa kutosha weekend unaweza kuta inakupa kipato cha kutosha maana inakodishwa sana.Hata kama malengo ni gar ya kutembelea sio mbaya ikikupa hela ya mafuta na service. Na pia Noah inavumilia sana barabara zenye mashimo.