everlenk
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 11,628
- 15,027
Habari wana JF,Nina dada yangu ambaye ni mjamzito na mimba yake ina miezi 11,lakini cha ajabu yuko fiti kabisa na hana dalili zozote za kusikia uchungu, tumeenda hospitalini Madaktari wakaona afanyiwe upasuaji tu lakini imeshindikana kwani kila akitakiwa kufanyiwa presha inapanda sana na kupewa maji ya uchungu imeshindikana hayakufanya kazi ,Sasa ameambiwa arudi tu nyumbani mpaka pale atakapojisikia kuumwa,Hii ni mimba ya pili ingawaje hata ile ya mtoto wa kwanza ilipitiliza hivihivi ikabidi afanyiwe upasuaji na ilikuwa salama kabisa hakuwa anapandwa na presha kama sasahivi.Naombeni ushauri jamani hili ni tatizo gani na husababishwa na nini? Na tiba yake ni nini?Mungu awabariki.