Ushauri tafadhali

Ushauri tafadhali

Joined
Aug 17, 2009
Posts
60
Reaction score
4
Ikiwa mmekuwa na tatizo la muda mrefu na mwenzi wako,mmejitahd kulitatua ila linaonekana halitoisha,ukaamua kupotezea.Ila imetokea tatizo hilo limekupelekea wewe upunguze upendo kwa mwenzio.Je ni sahihi kumueleza hisia zako kuwa upendo umepungua?au inaweza kuleta shida zaidi?.
 
ni sahihi kusema
na ni sahihi zaidi 'kutatua' hilo tatizo
ikishindikana mpeana 'space' kwa muda ili kila mtu
atafakari kivyake ili kufikia muafaka...
 
uwazi na mawasiliano anuai baina ya wenzi ndo nguzo ktk mahusiano yoyote duniani..
 
@the boss na gozo,kila m2 anaamini tofauti ktk hilo jambo(tatizo lililopo),na mwenzio anakuambia yuko sahihi ilhali wewe ukiangalia kwa undani unaona si sahihi,na linasumbua kwa muda mrefu,mmezungumza na kuzungumza ila mwenzio anasema ok nitalifanyia kazi ila sasa inazidi na hakuna changes hata kidogo,na uongo umeanza kuingia sasa,
 
vipi ikiwa mko kwenye ndoa?

Hujasikia ndoa zilizovunjika Bujibuji!? Huwa zinasababishwa na hali kama hii, kwamba kuna tatizo ndani ya ndoa ambalo linamfanya mmoja apunguze upendo na mwenzie pamoja na kuahidi atalishughulikia lakini hakuna improvement yoyote matokeo yake kila mtu anakuwa kivyake vyake na hatimaye mmoja anasema mimi ndoa basi.
 
Ikiwa mmekuwa na tatizo la muda mrefu na mwenzi wako,mmejitahd kulitatua ila linaonekana halitoisha,ukaamua kupotezea.Ila imetokea tatizo hilo limekupelekea wewe upunguze upendo kwa mwenzio.Je ni sahihi kumueleza hisia zako kuwa upendo umepungua?au inaweza kuleta shida zaidi?.

Sasa hapa ni swala la kuwa fair tu aisee, kwa kuwa mmejitahidi sana pamoja kulitatua na unadai linaonekana halitaisha, na wewe haukotayari kumpenda kwa moyo wote(kwani upendo umesha anza kupungua) akiwa na hilo tatizo, muambie tu ukweli, kwamba unampenda sana na ungependa mpendane hadi mwisho wa maisha yenu, Lakini haupendi kumuumiza moyo wake kwani upendo wako kwake siyo kama zamani wakati akiwa fresh na mungu ndo anapanga kila kitu kwa hyo akubali matokeo na mungu amjalie ampate mwingine atakae vumilia hiyo issue. itamuuma sana lakini ndo long term solution, vinginevyo unamuibia tu mwenzio
 
Labda ungemueleza kinagaubaga jinsi ambavyo upendo wako unapungua kwa sababu ya hilo tatizo. Ila usiishie hapo, kubalianeni kuwa flexible. Mkutane katikati ya solution. Namaanisha usifanye kosa looote kuwa lake. Kanza ujue kwa nini anafanya hivyo,na mabadiliko yawe taratibu huku ukimpa support.mfano kama ni mlevi sana,badala ya kunywa bia 15, anywe 5. Kama ni sigara badala ya pakiti kwa siku,basi avute kadhaa. Ila mueleze unashindwa kuendelea kuvumilia
 
Gozo nakuomba tu.. Badili hiyo avator yako ki ukweli inachefua sana
 
Yamenikuta kama hayo,unakuta mtu amekosea lakini ni mbishi kukiri makosa na kuomba msamaha utadhani atakufa akifanya hivyo.la msingi ni kuachana nae atakuja kupa presha za masaburi bureee
 
Kuna tatizo lingine ni human weakness ya mtu hawezi kuliondoa hata iweje probably nawe unayo yanayomkhera vile vile
SOLUTION: kama ni uchumbani mtaangalia if so mwaweza achana kama ni NDOA kuna usuluhishi mwingi mtaupitia lakini kumuacha na unajua hiyo ndo weakness yake ni kumwonea sema jaribu kumpa mkakati wa kumsaidia...mifano ya matatizo ni Hasira nyingi,wivu sana,carelessness,ukali, nk sasa msaidiane sio kumkimbia
 
Kama hamjafunga ndoa mnaweza tengana ila kama mko ndoani inabidi kusameheana..kuna makosa mengine hayakiriki kirahisi ila mnaweza anza upya ..msamaha ni jambo jema kwenye mahusiano ikiwa wote mnazungumza lugha moja(mnapojadili hamrushiani maneno)samehe na sahau omba Mungu akupe kifua chepesi maana ukikaa na hasira bible inasema ni wapumbavu peke yao wanaokaa na hasira,ni vizuri kama wewe ndio umekosewa tambua mwenzio sio malaika na hakukusudia kukuumiza ..huwa inatokea upendo kupungua ila ukishasamehe unarudi wenyewe wala hutajua imekuwaje.na utakapomsamehe epuka kuongelea tena hilo jambo hii itamfanya ajirudi na atafil guilty
 
Back
Top Bottom