Sio mahali pake hapa.
wewe umekariri hili jukwaa ni mambo ya mapenzi tu,Mahusiano na Urafiki siyo mahala pake eti?
Hapana itakuwa umenielewa vibaya ila swala la msingi ungeniuliza ni sehemu gani sahihi ni hayo tu.
Kwa sababu aliyeiba nguo ni mtoto cha muhimu ni watu wazima kukaa chini wakaongea yakaisha. Kama ni nguo anaweza aka nunua na kujilejesha.
Mwambie huyo rafiki yako amshauri rafiki yake jinsi ya kumlea mtoto ili asiendelee na tabia za wizi.
Lakini hiyo ni ishu ndogo.
wewe umekariri hili jukwaa ni mambo ya mapenzi tu,Mahusiano na Urafiki siyo mahala pake eti?
Hamna nini wala nini,hiyo sredi hapa siyo mahala pake. Over.
Malezi ya watoto ni ya jumuiya (staki kuuliza kwa nini majirani hawapatani). Kwa faida ya mwanae, amkamate mkono ampeleke kwa hao jirani. Wamkalishe chini, tena achapwe na wazazi wote wawili. Na wamuambie akiendelea kuiba kuna siku ataishia na tairi ya shingo. Kuna video humu ya mwizi akichomwa, wamuonyeshe kwa pamoja manake wanalea ufa watajenga ukuta.
mi sijaelewa sred yetu au futari imenitoa akili nin?
duh achapwe na wazazi wote wawili?
duh....iliwahi kukutokea hiyo?
sipati picha lol
Ofcoz ilinitokea. Nilimu-imitate jirani, akanicharaza. Nikadhani nimeonewa nikaenda kuhadithia home. Mama alikamata mkono tu, tukaenda kugonga hodi. Nikahojiwa, mama nae akanipa mboko zangu 3 mbele yake. Nikaomba msamaha. Huwa namkumbusha huyo neighbour anacheka sana!
sasa fimbo za utotoni mnazirudisha kwa innocent children naona lol