Habari,
Naombeni kujuzwa kisheria katika hili.
Je, inawezekana kufungua kesi ya madai katika mahakama ya wilaya na kisha mimi mdai nikaweka wakili wa kuniwakilisha katika kesi hiyo pasipo mimi kuhudhuria mahakamani kila wakati wa kesi? Sababu ya kutohudhuria ni labda niko mbali na kesi iliko, labda Kigoma na kesi iko Dar! Na hiyo ni kutokana na uendeshaji wa kesi kuwa ni wa kusikiliza na kuahirishwa mara kwa mara?
Natanguliza shukrani.