Mwenzenu nilipata ajali mwaka jana tar 24/10 ambapo nilianguka na baiskeli huko Iringa. Nilivunjika sehemu ya nyonga karibu na kiuno katika mguu wa kushoto.Nimekwisha hudhuria hospitali tofauti nilianzia hospitali ya mkoa wa mbeya, rufaa ya mbeya, CBRT, AMANA. Hivyo kutokana na mwingiliano wa shughuli zangu binafsi nilishindwa kufuatilia matibabu yangu kikamilifu mpaka mwisho. Mwezi march nilienda CBRT hapa dsm wakaniambia hawawezi kuweka chuma hiyo sehemu kwa vile nimechelewesha hivyo inabidi nifanyiwe 'hip replacement' ambapo gharama yake ni dola 5900. Hivyo mwezi huu nilienda Amana ili wanipe transfer ya muhimbili ili nione majibu yao. Hivyo waliniambia ngoja wachunguze kwanza wao, wakaniambia nikapige scan pale muhimbili nikawarudishia hapo Amana daktari akaniambia nyonga imekufa hivyo natakiwa niwekewe nyingine. Hivyo kanambia nikiwa tayari atanipa transfer muhimbili. Jamani naombeni kwa ushauri wowote au kama kuna daktari wa mifupa unayemufahamu pale muhimbili nipate ushauri wake hasa upande wa gharama? Nisaidieni mkulima mwenzenu!