Ushauri: TAKUKURU ivunjwe, haina manufaa yoyote bali inaongeza gharama za uendeshaji wa serikali

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) au PCCB ivunjwe maana inaiongezea serikali gharama za uendeshaji. Manufaa yake ni kidogo sana, taasisi zingine ndani ya serikali hii ya JMT zinaweza kufanya majukumu yanayofanywa na PCCB.

Nina miaka 7 ndani ya serikali, sijawahi kuona afisa wa PCCB anakuja kufuatilia manunuzi yanayofanywa na ofisi yetu direct au yaliyofanywa na mzabuni licha ya kuwa kwa nature ya taasisi yetu manunuzi yanafanyika kwa kiwango kikubwa.

Wakiagizwa na Waziri mkuu au waziri wa wizara husika waje wakague au waende ofisi fulani wakague hesabu za kihasbu ndani ya dk 30 wamefika.

Ni taasisi inayosubiri amri kutoka juu kila leo. Licha ya kuwa na authority ya kuruhusiwa kukagia ofisi zote za umma hata binafsi lakini huoni wanafanya hivyo.

Wakijitahidi sana basi wataenda shule na kuhamasisha wanafunzi wajiunge na anti corruption league . Na vijana wakidanganyana kuwa wataweza kuajirika PCCB kwa vyeti vile basi wanajazana.

Rushwa ndani ya Afrika huwezi kupambana nayo kwa kuelimisha bali kwa mkono wa chuma (ufuatiliaji kwenye field).

Ifutwe kabisa au ifumuliwe iundwe upya
 
Huku Africa taasisi kama hizi huwa hazina meno na wanasiasa wanafanya hivyo kwa makusudi ili wazitumie kwa manufaa yao na pia zisije kuwang'ata wenyewe. Wewe ulishaona wapi Taasisi ambayo iko professional inatumwa eti nendeni pale haraka muanze uchunguzi?? Hivi unaweza kumuamuru daktari kwamba haraka mfanyie oparesheni huyu mgonjwa?
 
Tatizo la Chama kimoja kutawala miaka yote
Hakuna wa kubadili kitu mpaka mabadiliko yawepo
Hapo napo inatakiwa wanaojielewa na kusimamia maslahi ya nchi na sio Chama au ubinafsi

Bado najiuliza kwanini viongozi wanaoingia madarakani wanabadili badili watu tu badala ya kubadili sheria na mambo yasiyokuwa na maslahi na Taifa?

Hapo mleta Mada una hoja ya msingi sana Kama watakuelewa maana huwezi kuwa na watu unaofikiria wanaweza kukamata wala rushwa wakati wengi wao wanakula pia
 
Ni taasisi inayosubiri amri kutoka juu kila leo. Licha ya kuwa na authority ya kuruhusiwa kukagia ofisi zote za umma hata binafsi lakini huoni wanafanya hivyo.
Naunga mkono hoja, PCCB haifanyi kazi yoyote, yaani ni mamlaka ambayo ipo kama picha, wafanyakazi wanalipwa mishahara pasipo kufanya kazi yoyote. Hata hizo kazi wanazoagizwa na waziri mkuu au wanasiasa wengine, bado huwa hazitekelezeki, yaani mwisho wake haujulikani. Walimhoji Mbowe masaa kibao, walimhoji mzee wa mabendera Kangi Lugola na hakuna kilichoendelea mpaka leo.. upotezaji tu wa fedha na muda. IVUNJWE
 
Hongera mleta hoja Kwa hoja Yako. Niliwahi andika humu juu ya uundwaji wa taasisi juu ya taasisi. Hii maana yake ni takukuru pamoja na polisi na mahakama ziundiwe chombo kimoja Cha kuwahakiki utendaji wao.
Hili halitakuwa la kwanza nchini kwani walimu Wana vyombo vilivyoundwa kisheria kufuatilia utendaji wao wa Kila siku na Kwa mahakama, polisi na takukuru waundiwe chombo Cha kuwafuatilia.
 
Mtoa mada, nakushauri utafute mahojiano ya Dr Hosea (aliyewahi kuwa mkurugenzi wa pccb ) na radio ya UN. Katika mahojiano hayo aliulizwa ni nini kinaikwamisha pccb, alilijibu kwa ufasaha. Na hizo sababu alizozitoa bado ziko valid hadi leo
 
Naunga mkono hoja

Nitarudia tena...
 
Habari!

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) au PCCB ivunjwe maana inaiongezea serikali gharama za uendeshaji. Manufaa yake ni kidogo sana, taasisi zingine ndani ya serikali hii ya JMT zinaweza kufanya majukumu yanayofanywa na PCCB.

Nina miaka 7 ndani ya serikali, sijawahi kuona afisa wa PCCB anakuja kufuatilia manunuzi yanayofanywa na ofisi yetu direct au yaliyofanywa na mzabuni licha ya kuwa kwa nature ya taasisi yetu manunuzi yanafanyika kwa kiwango kikubwa.

Wakiagizwa na Waziri mkuu au waziri wa wizara husika waje wakague au waende ofisi fulani wakague hesabu za kihasbu ndani ya dk 30 wamefika.

Ni taasisi inayosubiri amri kutoka juu kila leo. Licha ya kuwa na authority ya kuruhusiwa kukagia ofisi zote za umma hata binafsi lakini huoni wanafanya hivyo.

Wakijitahidi sana basi wataenda shule na kuhamasisha wanafunzi wajiunge na anti corruption league . Na vijana wakidanganyana kuwa wataweza kuajirika PCCB kwa vyeti vile basi wanajazana.

Rushwa ndani ya Afrika huwezi kupambana nayo kwa kuelimisha bali kwa mkono wa chuma (ufuatiliaji kwenye field).

Ifutwe kabisa au ifumuliwe iundwe upya

Huku Afrika taasisi kama hizi huwa hazina meno na wanasiasa wanafanya hivyo kwa makusudi ili wazitumie kwa manufaa yao na pia zisije kuwang'ata wenyewe. Wewe ulishaona wapi Taasisi ambayo iko professional inatumwa eti nendeni pale haraka muanze uchunguzi?? Hivi unaweza kumuamuru daktari kwamba haraka mfanyie oparesheni huyu mgonjwa?
Taasis nyingi sana zinaongezea serikali mzigo mkubwa wa uendeshaji, kwakuwa zinafanya majukumu yanayo fanana!.

PCCB wanashikaga watumishi wa ngazi za chini tu, huu ndio udhaifu wao mkubwa, lakini kazi wanafanya.

Me nashauri CAG aungane na mkaguzi wa ndani au Mkaguzi wa ndani awe pamoja na CAG, hii dhana ya kusibiri mwisho wa mwaka, ni uonezi kwa watumishi, huwezi fanya kazi mwaka mzima bila kukosea, wakaguzi wengine hawanaga simile, jambo dogo wanalikuza, lakini kama angekuwepo wakati jambo hilo linafanyika pengine angeshauri.

Hawa watu wa CAG wangeambatana na hizi ofisi moja kwa moja kuliko kutegeshea mwisho wa mwaka, nadhan kusingekuwa na haya tunayo yaona sasa.

watumishi wananyanyasika sana, unakuta mtu hata kama hausiki anajumuishwa kisa tu mkaguzi kamtaja!

Tunasafari ndefu sana!
 
Mtoa mada, nakushauri utafute mahojiano ya Dr Hosea (aliyewahi kuwa mkurugenzi wa pccb ) na radio ya UN. Katika mahojiano hayo aliulizwa ni nini kinaikwamisha pccb, alilijibu kwa ufasaha. Na hizo sababu alizozitoa bado ziko valid hadi leo
Sasa huu ni undezi, kwa nini wewe usiziweke hapa hizo sababu za Hosea?
 
Kuwa na Takukuru ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi ,naingia mkono hoja ifutwe pesa ikafanyie shughuli nyingine .

#Ova
 
Habari!

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) au PCCB ivunjwe maana inaiongezea serikali gharama za uendeshaji. Manufaa yake ni kidogo sana, taasisi zingine ndani ya serikali hii ya JMT zinaweza kufanya majukumu yanayofanywa na PCCB.

Nina miaka 7 ndani ya serikali, sijawahi kuona afisa wa PCCB anakuja kufuatilia manunuzi yanayofanywa na ofisi yetu direct au yaliyofanywa na mzabuni licha ya kuwa kwa nature ya taasisi yetu manunuzi yanafanyika kwa kiwango kikubwa.

Wakiagizwa na Waziri mkuu au waziri wa wizara husika waje wakague au waende ofisi fulani wakague hesabu za kihasbu ndani ya dk 30 wamefika.

Ni taasisi inayosubiri amri kutoka juu kila leo. Licha ya kuwa na authority ya kuruhusiwa kukagia ofisi zote za umma hata binafsi lakini huoni wanafanya hivyo.

Wakijitahidi sana basi wataenda shule na kuhamasisha wanafunzi wajiunge na anti corruption league . Na vijana wakidanganyana kuwa wataweza kuajirika PCCB kwa vyeti vile basi wanajazana.

Rushwa ndani ya Afrika huwezi kupambana nayo kwa kuelimisha bali kwa mkono wa chuma (ufuatiliaji kwenye field).

Ifutwe kabisa au ifumuliwe iundwe upya
Ilikuwa na nguvu kipindi Cha magu,baada ya hapo ukienda wanakuambia sisi tunashulikia mtu aliyekamatwa na siyo kuchunguza.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Kama unapima "perfomance" basi taasisi nyingi sana za serikali zinapaswa kuvunja maana hazina tija zaidi ya watu kula mishahara ya bure na kutumia bure fedha za walipa kodi tu.

Kizaramo wanasema, perfomance based na result oriented, siku tutakayojua maana ya hivi vitu n kuajiri pamoja na kupima watu wetu kwa kutumia tools hizo basi tutakuwa tumefaulu kwa kiasi kikubwa.
 
Back
Top Bottom