Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Uchaguzi wa viongozi wa TFF umevurugika.Sasa Serikali na FIFA wanaingia na kutoka TFF kutoa maelekezo,ushauri na maagizo kwa uongozi wa sasa wa TFF ulio chini ya Leodgar 'Chilla' Tenga. Kila mtu anasema lake.
Tatizo lilipoanzia
Tatizo lilianza pale Jamal Malinzi na Michael Wambura walipochujwa na kutupwa nje toka katika kugombea nafasi za Rais na Makamu wa Rais wa TFF kama walivyotajwa. Walijaribu kukata rufaa zao ndani ya mamlaka za TFF bila mafanikio. Sasa wanalalama kila kona: Serikali,CAF,FIFA na kwa jamii kwa ujumla. Wamesababisha uchaguzi wa TFF usijulikane unafanyika lini.
Ninachokiona
Ninauona mchezo huu wa kuharibu uchaguzi wa TFF kama mchezo unaoratibiwa na uongozi wa sasa wa TFF ili uendelee kuwepo madarakani kwa kipindi kirefu zaidi. Ni mchezo mchafu wa kisiasa michezoni. Soka la Tanzania linaelekea hata kufungiwa kimataifa kwakuwa sasa Serikali inaingilia masuala ya kimichezo kinyume na taratibu za FIFA. Tukifungiwa,nani atalaumiwa?
Kwanini?
Kwanini akina-Malinzi wasiachwe wagombee na wakataliwe na wapiga kura ndani ya TFF? Kwanini wanaonekana kama wakigombea tu basi watashinda;kwani hawawezi kushindwa?
Cha kufanya
Ni kuwarejesha wagombea waliondolewa 'kwa mizengwe' na uchaguzi ufanyike.Ikilazimu,ipangwe mizengwe ya kiuchaguzi ili wagombea hao=-Malinzi na Wambura wasishinde Urais wala Umakamu wa Urais TFF.Wakishinda,tukubali matokeo.
TFF ishaurike hivi