USHAURI: TFF ifanye hivi

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Uchaguzi wa viongozi wa TFF umevurugika.Sasa Serikali na FIFA wanaingia na kutoka TFF kutoa maelekezo,ushauri na maagizo kwa uongozi wa sasa wa TFF ulio chini ya Leodgar 'Chilla' Tenga. Kila mtu anasema lake.

Tatizo lilipoanzia

Tatizo lilianza pale Jamal Malinzi na Michael Wambura walipochujwa na kutupwa nje toka katika kugombea nafasi za Rais na Makamu wa Rais wa TFF kama walivyotajwa. Walijaribu kukata rufaa zao ndani ya mamlaka za TFF bila mafanikio. Sasa wanalalama kila kona: Serikali,CAF,FIFA na kwa jamii kwa ujumla. Wamesababisha uchaguzi wa TFF usijulikane unafanyika lini.

Ninachokiona

Ninauona mchezo huu wa kuharibu uchaguzi wa TFF kama mchezo unaoratibiwa na uongozi wa sasa wa TFF ili uendelee kuwepo madarakani kwa kipindi kirefu zaidi. Ni mchezo mchafu wa kisiasa michezoni. Soka la Tanzania linaelekea hata kufungiwa kimataifa kwakuwa sasa Serikali inaingilia masuala ya kimichezo kinyume na taratibu za FIFA. Tukifungiwa,nani atalaumiwa?

Kwanini?

Kwanini akina-Malinzi wasiachwe wagombee na wakataliwe na wapiga kura ndani ya TFF? Kwanini wanaonekana kama wakigombea tu basi watashinda;kwani hawawezi kushindwa?

Cha kufanya

Ni kuwarejesha wagombea waliondolewa 'kwa mizengwe' na uchaguzi ufanyike.Ikilazimu,ipangwe mizengwe ya kiuchaguzi ili wagombea hao=-Malinzi na Wambura wasishinde Urais wala Umakamu wa Urais TFF.Wakishinda,tukubali matokeo.

TFF ishaurike hivi
 
Mkuu PETRO E.Mselewa tatizo la uchaguzi katika TfF ni KATIBA!! Hata wakirejeshwa tatizo linakuwa ni wajumbe wanaopiga kura. Ni kakikundi kadogo kanakoshikiwa akili na hao jamaa wa ilala na kanahongeka kwa mfuko wa mtu moja tu!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu PETRO E.Mselewa tatizo la uchaguzi katika TfF ni KATIBA!! Hata wakirejeshwa tatizo linakuwa ni wajumbe wanaopiga kura. Ni kakikundi kadogo kanakoshikiwa akili na hao jamaa wa ilala na kanahongeka kwa mfuko wa mtu moja tu!

mkuu hapa kirusi ni Tenga kwani wakati yeye anagombea mambo yalikuwa safi ila na yeye anataka kuweka watu wake na kufanya mambo yawe kama yalivosasa kikubwa hapa ni tenga kuondoka na kuiachia tff kiroho safi na kama alikuwa na mawazo ya kuongoza CAF imeshakula kwake kakosa vyote sasa anataka kuharibu..

kuhusu FIFA kuingilia uchaguzi ni baada ya wao kina tenga kwenda kuilalamikia FIFA na kujifanya wanaingiliwa wakati si kweli hawa ndo mahasidi wakubwa wa soka hapa tanzania..

tenga nenda tuachie tff yetu..
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…