Ushauri :TIN moja Biashara mbili?

kokudo

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Posts
2,571
Reaction score
1,760
Naomba mwenye kujua TRA wanakubali mmiliki mwenye TIN moja akaitumia kwenye Biashara zaidi ya moja? je utaratibu wa malipo ya KODI utakuaje.

Naomba kuwasilisha
 
Naomba mwenye kujua TRA wanakubali mmiliki mwenye TIN moja akaitumia kwenye Biashara zaidi ya moja? je utaratibu wa malipo ya KODI utakuaje.

Naomba kuwasilisha
Asee mi pia nahtaj sana kufaham hii kitu
 
Yaani ni sawa unamiliki namba ya voda,unatakiwa kuwasiliana na mtu wa Airtel au halotel halafu unaanza kujiuliza hivi itawezekana kweli how?

Ni unatakiwa ujue tu TAX IDENTIFICATION NUMBER(TIN) ni utambulisho wako Mlipa Kodi.

Wanachofanya kubranch out kopi za tin certificate tu.
 
Inawezekana unachotakiwa ni kwenda tra wilaya yako ambako file lako lipo omba branch Tin.

Kuhusu makadirio mfano biashara ya kwanza kodi unalipa 800,000 kwa mwaka wakati wa makadirio wanajumlisha tawi jipya labda 400,000
.

Naomba mwenye kujua TRA wanakubali mmiliki mwenye TIN moja akaitumia kwenye Biashara zaidi ya moja? je utaratibu wa malipo ya KODI utakuaje.

Naomba kuwasilisha
 
Tin nihiyo hiyo moja ila leseni yabiashara ndio itakubidi kila biashara/ofisi ijitegemee
 
Tin nihiyo hiyo moja ila leseni yabiashara ndio itakubidi kila biashara/ofisi ijitegemee
Sawa tin ni moja tu lakini lazima tra wajue kuwa inatumika kwenye biashara zaidi ya moja, na kodi itatozwa kwenye biashara zote mbili, kila biashara itakuwa na file lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…