Ushauri: TRA ifanye hivi kuongeza mapato

Ipi nafuu Bei ni mbili ya risiti ni laki Tano ya bila risiti ni laki nne uamuzi ni wako.
Kama tunanufaika na Kodi unaachaje kuilipa
Solution yangu ni ku solve hasa kwa wasiodai risiti kabisa. Kama atakupunguzia na kukupa risiti its OK. Kumbuka ukidai risiti unarudishiwa pesa yako ambayo ni 1% ya VAT uliyotozwa.
 
Kwasababu utapata sms ya risiti papohapo, utaona bei aliyokuandikia ikiwa tofauti unamwambia akuandikie ya kiasi kilicho pungua papohapo
Sawa utafanya ivyo ila kumbuka watakwambia waandike bei ndogo kwenye risiti ilalf akupunguzie bei apo ameshawapata wengi sana maan watu huwa wanapenda kupunguziwa chakifanya nikuwapa elimu watanzania juu yakudai risiti yenye bei sahihi kwaajili yakuijenga tanzania
 
Nikupongeze kwa andiko zuri japo wengi linaweza kuwa limetukera ila umeweza weka wazi mambo ya msingi n mazuri. Mimi nionavyo EFD ingeenda mbali zaidi kila muuzaji akawa na mashine ya EFD kwa kuzingatia kwa sasa kuna ile VFD ambayo inasemekeana huna haja ya kutoa risiti sababu imeungwa kwenye simu unaweza tuma risiti kwa whatsapp au kama mtu huna smart phone ukanunua kiprinta kidogo ukatoa. Hapa changamoto ya kusema kodi kubw itapungua na hata kujikadiria kodi mwenyewe inatkuwa rahisi maana kila mmoja atajua ni kiasi gani kapata na kodi kiasi gani atalipa. Ikiwa kila mtu atatumia hii mashine naamini kabisa hata ile kamatakamata tunaweza kutokutana nayo maana kila mtu atakuwa na risiti. Ombi langu kwa Serikali na TRA kwa ujumla kuendelea kutoa elimu ya matumizi haya ya EFD /VFD ili sisi sote wananchi tuweze fahamu umuhimu na wajibu wetu kwenye kudai na kutoa risiti. Mimi zamani kablaya kuanza kutumia mashine hii niliwahi ambiwa inakata 18% sikuelewa kumbe wenzangu walimaanisha VAT . Pia tra naomba sana kuna hiki kilio cha kutujuza namna ambavyo ukinunua hii mashine nafahamu kuna kurejeshewa garama ya manunuzi tunaomba mlitolee ufafanuzi pia hili
 
Iongeze kukusanya mapato yapi? Unataka wakusanye mpaka damu?.

Maana kila mwaka inavuka malengo ya ukusanyaji. Mfano kama mwaka huu malengo ni kukusanya elfu 20 wanavuka mpaka elfu 40.

Kila mwaka wanavuka malengo ndio ujue wananchi au mfanyabiashara hakwepi kodi,ila Vita yote uliyoizingumzia kati ya TRA na wafanyabiashara,kuna mambo mengi ambayo sina muda wa kuyaandika yote. Yanayombana mfanyabiashara.

Pia kuna swala la mazingira ya upangaji matokeo.

Swala la mashine. Kwanza ilitakiwa TRA wenyewe ndio wawe nazo hizo mashine wagawe bure kwa wafanyabiashara,ksbb wao ndio wenye uhitaji wa hizo mashine bila kumuonea mtu. Pia matengenezo yake iwe juu ya TRA.

Ukija kwenye swala la kutoa risit. Wewe ulieleta huu Uzi japo sijasoma wote lakini unaweza usiwe unaifahamu hata biashara ya kuuza nyanya tu. Ingia kwenye biashara kwa hapa Tanzania ndio utauona mziki wake. Ukitoa rist kwa 💯 ujue unaenda kufunga biashara yako.. Huo ndio ukweli. Na semina zote tunazokaa na TRA wanaelezwa hili pia. Na ndio maana wananchi wengine hawadai risit kwa nguvu ksbb tunaishi nao wanajua madhira anayopitia mfanyabiashara wa Tanzania kwa upande wa kodi.

Kwa ujumla kodi za Tanzania nyingi ziko juu kuliko nchi zote zinazotuzunguka. Nafikiri hatuna wataalam wazuri kuhusiana na mambo ya kodi. Au ni makusudi ya maafisa.

Mfano mzuri wewe na rafikiako Mmalawi mmeagiza magari aina moja labda Toyota corolla kila mmoja la kwake. Kule mmenunua kwa kila mmoja milioni 4 labda. Gari zote mbili zikasafirishwa mpaka hapa bandarini Dar. Wa Malawi akalichukua gari lake akaenda kulipia upande wao wa Malawi milioni 2 kwa rate ya Tsh. Gari hilo hilo kwa hapa bongo unaweza kulipia kodi milioni 7,8 hadi 9. Kwa gari hilo hilo. Wakati yule Mmalawi kapitisha kwenye bandari yetu,sisi wenye bandari badala tunufaike nayo lakini matokeo yake ndio hivyo

Mfano mwingine kontena la vitenge kwa Zanzibar haizidi milioni 38 mpaka 40. Kenya hivyo hivyo. Zambia milioni 35. Kwa hapa bongo ni milioni mia 300. Wakati ni nchi za ukanda mmoja. Na sisi Watanzania ilipaswa tunufaike ksbb tuna bandari.

Mimi nafikiri uanze kuyazungumzia haya kwanza ili angalau tuwe sawa kwenye viwango vya kodi na nchi zingine.
 
Mambo uliyoyaongea yanapigiwa kelele miaka nenda,rudi.Hajuna anayesikiliza.Inatia uchungu sana,kama yangefanyiwa kazi tungekuwa mbali ssna kimaendeleo.Huwa inafukia mahala naanza kuamini huenda kunablaana inafanya kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…