Ushauri: Tunza ngozi yako wakati wa uzee

Ushauri: Tunza ngozi yako wakati wa uzee

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Umri ni kigezo kikubwa kinachoweza kusababisha mabadiliko katika ngozi. Mabadiliko makubwa zaidi huonekana wakati wa kuelekea uzeeni, ambapo huanzia miaka 40 na kuendekea.
Katika kipindi hiki utaweza kubaini mabadiliko makubwa ikiwamo ngozi kukunjamana, hata kupoteza mng’ao wake wa asili uliokuwapo wakati wa ujana.
Vilevile ngozi inakuwa kavu na kupauka mno. Endapo utaanza kuona hali hiyo, epuka kupambana nayo kwa kutumia vipodozi vyenye kemikali.
Ingawa ni vigumu kukabiliana na hali ya uzee, lakini unaweza kuifanya ngozi yako kuwa na mwonekano mzuri, licha ya kuwa na umri mkubwa.
Fuata dondoo zifuatazo kuhakikisha ngozi yako inabaki na mvuto licha ya uzee ulionao au unaokaribia kukufika.
Kwanza zingatia mlo kamili kwa kula zaidi matunda, mboga za majani, maziwa na maji walau lita tatu hadi nne kwa siku.
Epuka ngozi yako ya uso kupigwa na mionzi ya jua mara kwa mara, kwani hilo huchangia kwa kiasi kikubwa kuidhoofisha na hatimaye kukunjamana.
Katika kipindi hiki, epuka kutumia vipodozi bila kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa masuala ya ngozi, wanaoweza kukushauri aina gani ya vipodozi inayoweza kuwa salama katika ngozi yako.
Tumia losheni zisizo na kemikali au kavu kupita kiasi kwani wakati wa uzee ngozi huwa na asili ya ukavu. Paka losheni itakayokuwa na mafuta yatakayolainisha na kung’arisha ngozi.


Source: MCL
 
Back
Top Bottom