Ushauri: Tuwe na Mkapa Day

Kwa mantiki hiyo Mwinyi, Kikwete day na Magufuli day zipo mbioni...sasa baada ya miaka 100 kizazi kitakachokiwepo kinakuwa ba days ngapi?
 
Kama unadhani kumpa siku mkapa ni jambo jema basi mtengee hiyo siku hapo nyumbani kwako.

Sisi usituhusishe kabisaaaa.

Wengine hata kuaga walipigwa pini.
 

Mkapa ni baba wa Demokrasia!

Niko nje ya nchi au nchini?
 
Kiwira coal mine
Nimezinduka kabla sijamaliza kuota ndoto.
 
dndagula,

Wazo zuri sana. Ingefaa iwe siku ile yalipotokea mauaji ya wale Wazanzibar January 2001.

Ni mtizamo tuu kama mzalendo, maana hata siku ya mtoto wa Afrika imeteuliwa kuwa ile iliyotokea mauaji ya watoto kule Soweto SA
Kama unadhani kumpa siku mkapa ni jambo jema basi mtengee hiyo siku hapo nyumbani kwako.

Sisi usituhusishe kabisaaaa.

Wengine hata kuaga walipigwa pini.
🤝
 
Mkuu ni wazo zuri lakini ninapofikiria idadi ya marais watano tulio nao hadi hivi sasa tukiweka memorial Day ya kila mmoja itakuwa ni vurugu tupu! Mfano Nyerere Day, Karume Day, Mkapa Day, Mwinyi Day, Jk Day, JPM Day na wengine watakaofuata! Sasa ikitokea wote wakafariki tarehe zinazofuatana maana yake tunawezajikuta tunakuwa na wiki nzima ya mapumziko na kusimamisha shughuli za serikali kwa ajili ya kuadhimisha public days za marais wetu! Ni kweli kila kiongozi hasa kwa ngazi ya urais na kwa vipindi vya miaka kumi madarakani ni lazima atakuwa na mengi aliyoyafanya japo kwa kuwezeshwa na rasilimali tulizo nazo pamoja na uwezo wake binafsi, lakini pia hatuwezi kujisahau kuwa nchi yetu Tanzania na watanzania walio wengi bado ni masikini, bado hatuwezi kusimama wenyewe na tukatekeleza miradi ya maendeleo bila mikopo toka kwa wahisani, zaidi ya yote tulio wengi maisha yetu ni ya kubangaiza, hata hiki kinachoitwa uchumi wa kati ukimuuliza mkulima kule Tandahimba au Kyela au Nsimbo au Ntendo kule Kalambo kwamba amejihisi mabadiliko gani anayoweza kusema ukuwaji wa uchumi huo umemgusa hana jibu la kukupa! Hivyo ni lazima tuutumie muda wetu vizuri, kwa hili nashauri tu kwamba tufanye mjadala wa kitaifa itengwe siku moja tu kwa ajili ya kuwaenzi marais wetu wote na kila atakayetangulia mbele za haki anaunganishwa hapo!
 
Kabla hajavuta mlikuwa mnambeza tu na sifa zote kwa Jiwe kama ndo ameipokea nchi kutoka kwa Nyerere!

Hii nguvu ya soda, Mkapa tunamsahau mapema sana, yaani baada ya muda mfupi tu ujao.
 
Just Hahahaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…