Ushauri: UDART Mwendokasi kuwe na refund

Mshobaa

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2013
Posts
1,714
Reaction score
677
Salaam,

Hakika ukitaka kusafiri jioni kuelekea kimara kuanzia saa 11 na kuendelea kupitia Mwendokasi ujipange kisaikolojia, ukikata tickets kwenye vituo huwa hawakuambii hali ya usafiri ipoje, ukiingia kusubiria basi ndio kasheshe huanzia hapo.

Jana kwenye kituo cha magomeni mapipa nimeshuhudia kinamama wakiwa wanalalamika kukaa kituoni kwa zaidi ya masaa mawili bila gari kuwachukua hadi wakaamua kughairi na kwenda kutafuta njia nyingine ya kuwafikisha huko waendako, walipolalamika kwa wakatisha ticket warudishiwe hela ya nauli wanadai hilo haliwezekani kwani ukishakata ticket ndio basi tena.

Ombi langu kwa mamlaka husika hizi tickets zina muda wa kuingia na kutoka kwenye vituo hivyo basi kama muda umepita na sijapata usafiri kuwe na haki ya kudai hela yako ukatafute usafiri mwingine ili kuwa na huruma na hawa watu.
 
Mradi ulifeli kabla haujaanza baada ya kumuondoa MAXCOM.
Sasa hivi mkurugenzi UDART natekeleza ushari walipewa wa "kula usawa wa kamba yako" ila usivimbiwe!
 
Back
Top Bottom