Story live ila ya zamani: Baada ya kutoka JKT, best aliajiriwa Maji Ubungo. Akasaidiwa vijisenti na ndugu na kununua kiwanja Makongo. Enzi hizo hata usafiri kulikuwa hakuna hivyo alikuwa anasafiri kwa baisikeli kupitia Ardhi- UDSM mpaka kazini. Akajenga choo na chumba kimoja pembeni kabisa kiwanjani. Akitoka kazi au jioni mwenyewe anapiga tofari na kuchimba msingi. Zege na nondo alishonewa na kusaidiwa na ma technitian wa maji ambao walikuwa rafiki zake. Malipo ni bia za jioni pale kwake - palikuwa patupu bado. Obviosly, kila bidhaa alikuwa anaagiza na kupokea mwenyewe. Funzo: alikata cost za upangaji, cost za usafiri, vikao vya baa na sherehe zisizo na msingi, kula nyumbani, labour and specialists cost. Chukua uonalo linafaa.....