joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Ni wazi kwamba kwa muda mrefu tumekua tukilinganisha na kutunishiana misuli kati ya Kenya na Tanzania kwa kulinganisha maeneo mbalimbali ya kimaendeleo, kisiasa, kijamii na kimichezo.
Sasa hivi kila mmoja wetu hapa JF na nje ya JF raia wa hizi nchi mbili anayefuatilia kwa makini yanayotokea, tayari amepata jibu la huu mnyukano unavyoelekea, na hali ilivyo kati ya Kenya na Tanzania.
Binadamu tumeumbwa na mapungufu mengi, hasa sisi waafrika tumeumbwa na mapungufu ya kutokubali kushindwa na kukiri hadharani, ndio sababu ukiachana na Nigeria, Ghana na South Africa, Hakuna nchi ambako walioshindwa kiti cha urais wamekiri na kuwapongeza walioshinda, japo baadae wanakiri kwamba kweli walishindwa.
Ombi langu kwa sasa, ni vizuri kupunguza malumbano ya kulinganisha kwa lengo la kishabiki ili kuonekana upande mmoja ni bora kuliko upande mwingine, badala yake kujaribu kuonyesha yale ambayo tunahisi upande wa pili unafanya vizuri ili upande mwingine uweze kujifunza.
Mimi binafsi ningependa sana kujua na kujifunza kwanini bandari ya Mombasa inapata na kupokea mizigo mingi kuliko bandari ya Dar es salaam wakati bandari ya Dar es Salaam inahudumia nchi nyingi kuliko Mombasa?
Karibuni wadau kuchangia?